MTANGAZAJI

MAFUNDISHO YA KIROHO KWA MIJI MIKUU KUFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM



Uongozi wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato katika Unioni Misheni ya Kusini mwa Tanzania kwa kushirikiana na conferensi ya Mashariki na makanisa ya jijini Dar es salaam unatarajiwa kuendesha mkutano wa injili katika vituo 123 jijini humo kuanzia juni mosi hadi juni 21 mwaka huu.

Mkutano huo ambao ni utaratibu wa kanisa hilo duniani katika kuwafikia watu mbalimbali wa kada tofauti wanaoishi katika miji mikuu kwa kuwapatia mafundisho yahusuyo neno laMungu,Afya,Uchumi,Kaya na Familia pamoja na maombezi uliopewa kauli mbiu ya Utume wa Matumaini katika miji mikuu pia utarushwa na Morning Star Radio kila siku saa 2:15 usiku ambapo mzungumzaji atakuwa ni Mwenyekiti wa Unioni ya Kusini mwa Tanzania Mchungaji Magulilo Mwakalonge.

Taarifa ya Mkurugenzi wa Huduma wa Unioni ya Kusini mwa Tanzania Mchungaji Stephen Letta iliyotolewa leo kwa Morning Star Radio inaonesha kuwa katika vituo hivyo mkutano utakuwa ukifanyika kila siku saa 9 alasiri ambapo viongozi na washiriki wa makanisa watashiriki kufanikisha mkutano huo.




No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.