MTANGAZAJI

ARUSHA:POLISI JAMII WA SOKONI ONE WAGOMA BAADA YA KUTOLIPWA POSHO ZAOWakazi wa mtaa wa kanisani katika kata ya sokoni one jjijini Arusha wako katika hatari ya kukumbwa na matendo ya kihalifu kama wizi,uuaji na ongezeko la matumizi ya pombe haramu,kufuatia kugoma kwa polisi jamii ndani ya kata hiyo kwa madai ya kutolipwa posho zao

 Mmoja wa wananchi ambaye ni polisi jamii wa kata hiyo Bernad Ronga  amezungumza jana mei 27 na vyombo vya habari amesema kuwa wamefikia hatua hiyo ya kugoma kufuatia malimbikizo ya posho zao ambapo alieleza kuwa hawakulipwa tokea mwezi wa pili mwaka huu.

Kufuatia malalamiko hayo mwenyekiti wa polisi jamii na mkuu wa oparesheni ya Tokomeza uhalifu na madawa ya kulevya kata ya sokoni one ,Abed Mtengwe alikiri kuwepo kwa mgomo huo na hivyo alimua kutoa fedha zake kuwalipa vijana hao waliokuwa polisi jamii katika kata hiyo.

Pia ameeleza kuwa yapo mafanikio makubwa yaliyofikiwa kabla ya mgomo huo na iwapo hatua madhubuti hazitachukuliwa kuwarudisha vijana hao kazini  upo uwezekano mkubwa wa historia ya uhalifu na uovu uliokithiri kujirudi katika kata ya sokoni one.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.