IRINGA:UPUNGUFU WA WAUGUZI WAKWAMISHA HUDUMA ZA AFYA
Imebainika
kuwa Sekta ya afya mkoani Iringa imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya idadi
ndogo ya wauguzi na kusababisha wagonjwa kushindwa kupatiwa huduma muhimu na
wakati mwingine kupoteza maisha kabla ya kuhudumiwa.
Mganga
mkuu wa zahanati ya Ipogoro Bw Andrea Mwinuka amesema kuwa idara ya
afya mkoani Iringa inakabiliwa na changamoto hiyo, hivyo serikali itoe
msaada ili kuondokana na tatizo hilo.
Aidha
amewashauri wananchi kuendelea kuchangia mfuko wa jamii ili kupatikana fedha
zitakazosaidia kununua dawa za kutosha ili kupunguza tatizo la ukosefu wa dawa.
Mkoa wa
Iringa ni miongoni mwa mikoa inayokabiliwa na changamoto hiyo kwa baadhi ya
hospitali na zahanati jambo ambalo linasababisha muuguzi mmoja kuhudumia
wagonjwa wengi zaidi.
Post a Comment