PWANI:WANAUME WASHINDWA KUPIMA VVU
Imefahamika kuwa idadi kubwa ya wanaume walioko
katika ndoa Kibaha mkoani Pwani wameshindwa kujitokeza katika zoezi la upimaji
wa virusi vya ukimwi(VVU) na badala yake wanategemea majibu ya wake zao.
Akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo katika kikao cha
kawaida cha baraza la Madiwani wa mji wa Kibaha hivi karibuni Mwenyekiti wa
kamati hiyo, Sloom Baghmesh,amesema ni vyema wanaume nao wakabadilika na
kujitokeza kwenda kupima afya zao.
Baghmesh alibainisha kuwa sababu kubwa
inayotolewa na
baadhi ya
wanaume hao kushindwa kujitokeza kwenda kupima VVU ni hofu na kuongeza kuwa
inaonekana elimu ya kupima kwa hiari haijaeleweka vizuri kwa kundi hilo.
Kamati hiyo imekuwa ikitembelea vituo
mbalimbali vya
afya na kuelezewa changamoto ambayo inakwamisha jitihada za mapambano
dhidi ya ugonjwa huo.Kwa mujibu wa taarifa hiyo kati ya Januari hadi Machi
mwaka huu, jumla ya watu 2,746 wakiwamo wanaume 1,003 walijitokeza kupatiwa
ushauri na kupima afya zao.
Hata hivyo kati ya watu waliojitokeza 303 walikutwa na
VVU
wakiwamo
wanawake 217 na wanaume 86.Utafiti unaonesha kuwa miongoni mwa vichocheo vya
maambukizi ya VVU ni majumba ya video,picha chafu za ngono,unywaji wa
pombe,kutetereka kwa ndoa,mila potofu na tabia ya kufunga ndoa bila kupima.
Post a Comment