MTANGAZAJI

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI ASEMA MIGOGORO YA ARDHI INACHANGIA KUDIDIMIZA SEKTA YA MIFUGO TANZANIA

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi nchini Tanzania,Dk. Titus Mlengeya Kamani, amesema uharibifu wa mazingira na migogoro ya Ardhi hapa nchini,ndizo changamoto zinazorudidha nyuma sekta ya mifugo kuchangia pato katika uchumi wa Taifa.

Dk.Kamani amesema hayo hivi karibuni wakati akiweka jiwe la Msingi katika Ofisi ya kituo cha Mafunzo ya Mifugo Mabuki, Misungwi,Mkoani Mwanza.


Amesema, licha ya wafugaji wa Tanzania kuwa na idadi kubwa ya mifugo,bado ni masikini ambapo takwimu zinaonesha kuwa zinaonesha kuwa ,Tanzania ina ng’ombe milioni 22.8,mbuzi milioni 15.6,kondoo milioni 7.0 na kuku milioni 58,lakini hali ya wafugaji nchini humo ni mbaya na wanaishi maisha duni.


Kulingana na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, katika msimu wa mwaka 2011/2012 takribani ng’ombe milioni moja,mbuzi 771,967 na kondoo 179,289 wenye thamani ya shilingi bilioni 775.4 waliuzwa kwenye minada mbalimbali hapa nchini Tanzania.


Idadi ya ngombe 3,367 kondoo na mbuzi 4,060 wenye thamani ya shilingi bilioni 3.81 waliuzwa katika masoko ya nje,hususan nchini Comoro.


Aidha,tani 31.6 za nyama ya ng’ombe, tani 647 za nyama ya mbuzi na tani 151.8 za nyama ya kondoo zenye thamani ya shilingi bilioni 19.3 ziliuzwa nchini Kuwait na Oman.


Kufuatia hali hiyo,Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Dk.Kamani amewataka watendaji wa serikali kuzuia uharibifu wa mazingira na kuondoa migogoro ya ardhi,ili kuwezesha ufugaji wa tija hapa nchini.


Kanda ya Ziwa Viktoria nchini Tanzania inaongoza kuwa na idadi kubwa ya mifugo hapa,na ndiyo yenye kiwango kikubwa cha umasikini wa kipato.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.