MTANGAZAJI

MAHAFALI YA CHUO CHA CITY MEDIA CHA ARUSHA KUFANYIKA KESHO

Zaidi ya wanachuo mia moja ishirini na mbili wa kozi mbalimbali katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji cha CITY MEDIA COLLEGE cha jijini Arusha wanatarajia kutunukiwa vyeti vya kuhitimu kozi mbalimbali tukio ambalo litafanyika tarehe kesho April 11, 2014 katika viwanja vya chuo hicho.

Kwa mujibu wa Taarifa kutoka kwa mkurugenzi wa City Media College Ndugu Geofray Wambura chuo hicho kilianzishwa Rasmi mnamo januari tano 2011,kikiwa kinafundisha kozi za uandishi wa Habari, utangazaji pamoja na ualimu katika ngazi ya cheti na stashahada.


 Wambura amesema katika mahafali hayo mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa mkuu wa wilaya ya Arumeru ndugu Nyerembe Munasa Sabi.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.