MTANGAZAJI

BAADHI YA WAKAZI WA JIJINI DAR ES SALAAM WAHOFIA USALAMA WA MAKAZI YAO KUTOKANA NA MVUA

Ujenzi wa nyumba za makazi ya watu pamoja na ukosefu wa mifereji ya maji ya mvua kwa wakazi wanaoishi maeneo ya msasani jijini Dar  es salaam umelezwa kuchangia wakazi hao kuendelea kuishi kwa mashaka hasa kipindi hiki cha msimu wa mvua kutokana na maji kutuama nakufunga barabara huku maji mengine kuingia kwenye nyumba za wakazi hao
.
Baadhi ya wakazi wa maeneo hayo wamesema kuwa ujenzi holela wa nyumba karibu na miundo mbinu ikiwemo mifereji yakupitisha maji na utupaji wataka ovyo kwenye mifereji hiyo kuziba na pindi mvua inaponyesha maji hutuama nakufunga barabara kuu au kutafuta mweelekeo mwengine nakuingia kwenye nyumba za wakazi hao.


Mwandishi wa habari hii ameshuhudia kujaa kwa maji mengi baada ya mvua kunyesha kwa siku ya jana katika eneo la kati ya myfair plaza na hospitali ya TMJ kwenye barabara ya Mwai kibaki maji ambayo yalimaji yalisambaa katika makazi ya watu wanaoishi katika maeneo ya msasani na kusababisha usumbufu kwa wenye magari na waendao kwa miguu,hali ambayo pia imesababishwa na ujenzi wa daraja jipya katika eneo hilo.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.