MTANGAZAJI

WAKANDARASI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA

Wakandarasi nchini wametakiwa kuchangamkia fursa za ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali katika maeneo mbalimbali ili kurahisisha uwekezaji pamoja na kuleta wataalam wa kigeni ambao wanalipwa fedha nyingi 

Ushauri huo umetolewa na mwenyekiti uchumi wa kanda ya Tanga Chris Chae alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo mara baada ya kutembelea eneo la mradi wa viwanda vya uwekezaji zaidi ya ishirini kutoka Korea na Indonesia 

 Chae amesema kuwa licha ya Tanzania kutafuta uwekezaji bado kuna tatizo la wazawa hasa wenye utaalam wa kujenga majengo ya kibiashara kwenye maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji Bw Chris ameongeza kuwa hadi ifikapo mwezi wa sita mwaka huu wawekezaji hao watakuwa wamejenga viwanda vitano na ambavyo vitatoa ajira kwa watanzania zaidi ya elfu ishirini elfu.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.