MTANGAZAJI

JAMII YATAKIWA KUSAIDIA YATIMA

Watoto na walezi wa vituo mbalimbali vya kulea watoto yatima mkoani Arusha wameitaka jamii serikali na mashirika mbalimbali nchini Tanzania kujenga mazoea na tabia bora ya kutembelea vituo hivyo ili kujua na kutoa misaada kwa watoto hao ambao mara nyingi husahaulika kuwa nao wana haki ya kuishi sawa na mwanadamu yeyote. 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wa habari  wamesema kuwa jamii ya watanzania inapaswa kutazama kwa macho ya huruma watu wote wasio na uwezo ili kuwawezesha kuwa na maisha yenye amani na pengine kuwapatia mahitaji muhimu kama vile elimu,malazi bora,chakula na mavazi. 

Kwa upande wake William Fillemoni Msuya wa kituo cha Faraja kilichopo katika kata ya kimandolu mkoani Arusha ameeleza kuwa zipo changamoto nyingi zinazoikabili jamii hii hususani katika kituo chake kuwa wanakabiliwa na upungufu wa vyakula na fedha kwa ajili ya kuwalipia Ada ya masomo kwa watoto wanaolele kituoni humo,hivyo akaiomba jamii kuona kuwa ni jambo la hekima na busara kuwapa nafasi watu kama hawa wanaohitaji nguvu kutoka kwa wadau mbalimbali hapa nchini. 

Aidha walezi hao katika kituo cha Faraja wamelishukuru Kanisa la waadventista wasabato mjini kati Arusha kupitia idara ya vijana kwa kuonesha moyo wa upendo kupitia msaada wa vyakula,mavazi na maombi yaliyofanyika katika kituo hicho mapema machi 15 mwaka huku wakiomba , mpango huu uwe endelevu katika vituo vyote vya kulea watoto yatima hapa nchini.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.