MTANGAZAJI

WAHAMIAJI HARAMU WATATU TOKA ETHIOPIA WAKAMATWA TARIME

Jeshi la polisi Wilayani Tarime linawashikilia Wahamiaji haramu watatu kutoka nchini Ethiopia baada kukamatwa katika kijiji cha Kerende kata ya Kemambo.

Wahamiaji hao wamekamatwa machi 19 majira ya saa nne na nusu asubuhi wakisafiri kwa gari lenye namba za usajiri T.842 CRB Toyota Hiace gari la abiria kutoka Isbania Nchini Kenya wakielekea Wilaya ya Serengeti.


Kerende ambayo iko kaskazini mashariki mwa mkoa wa Mara iko mpakani mwa nchi ya Kenya kutokana na ukaribu huo wahamiaji hao walipata nafasi ya kupenya kuingia Tanzania.


Taarifa ya polisi kwa vyombo vya habari iliwataja waliokamatwa kuwa ni Thamrash Abdalah, Algeje Abdalah na Doudam Abdalah ambao umri wao haukufahamika kutokana na kutokujua kuongea lugha ya Kiswahili ama Kingereza.


Kamishina msaidizi wa jeshi la Polisi Mkoa wa kipolisi wa Tarime Rorya Justus Kamgisha alimeeleza kuwa hizi ni juhudi za wananchi kuonesha ushirikiano wa dhati kuhakikisha mtu ama watu wanaodhaniwa kuwa si raia ama hawafahamiki walikotoka watolewe taarifa kwa jeshi la polisi kwa kulinda usalama wa maeneo wanayoishi.


Na:Waitara Meng'anyi

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.