MTANGAZAJI

ARVs ZINAZUIA MAAMBUKIZI MAPYA YA UKIMWI

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI NAKOFA (NACOPHA), Bwana Vitaris Makuyula, amesema iwapo dawa za kupunguza makali ya UKIMWI (ARVs) zitatumiwa kwa miaka mitatu mfululizo zinazuia maambukizi mapya ya ugonjwa huo kwa mtu mwingine.

Bw Makayula ametoa kauli hiyo mjini Morogoro wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuondoa unyanyapaa kwa viongozi wa dini nawadau wengine kwa ufadhili wa shirika la marekani linalojihusisha na mapambano ya ugonjwa Ukimwi (UNAIDS.)


Naye mshauri mhamasishaji jamii kutoka shirika la kimataifa la UN AIDS,Yeronimo Mlawa, ametoa wito kwa viongozi wa kidini kuzungumzia athari za unyanyapaa kwa waumini wao nakuzikemea pale zinapotokea, huku akizitaja dawa za kulevya kuwa ni miongoni mwa kikwazo kikubwa katika kumaliza maambukizi mapya.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.