KWAYA YA KIJENGE SDA KUANZISHA MRADI WA DUKA NA UNUNUZI WA BUS
Kijenge SDA Choir wakiimba |
Miradi hiyo ambayo wadau wake wakuu ni kwaya ya waadventista wasabato kijenge unatarajiwa kuwanufaisha wapenzi wa nyimbo za injili hususan za waadventista wasabato kwa kuwa moja kati ya shughuli zitakazofanyika katika duka hilo ni pamoja na kudurufu nyimbo za kwaya mbalimbali kimkataba na kuziuza.
Akizungumza mapema jana na mwandishi wa habari hii, mkuu wa miradi wa Kwaya ya Kijenge Bi Nelly Mzava ameeleza kuwa bus hilo litakaponunuliwa litatumika kwa ajili ya safari za kwaya hiyo ambayo hufanya uinjilisti ndani na nje ya nchi ya Tanzania.
Fedha hizo zina tarajiwa kupatikana kutoka kwa kanisa,mradi wa nyimbo zitakazokuwa kwenye cd na dvd, pamoja na wafadhili mbalimbali nchini Tanzania watakaoshirikishwa.
Na Abel Kinyongo
Post a Comment