MTANGAZAJI

WENYEVITI WA VIJIJI VIWILI MWANZA MBARONI KWA TUHUMA ZA MAUAJI

Watu watano,wakiwemo Wenyeviti wa vijiji vya Fumagila Mashariki na Magharibi,wilayani Nyamagana,Mkoani Mwanza,wametiwa mbaroni na Jeshi la Polisi,kwa tuhuma za kumuua mtu mmoja kwa tuhuma za wizi wa debe la mpunga.

Imeelezwa na polisi kwamba Machi 10 mwaka huu,mwanaume ambaye hajafahamika jina na anakoishi, mnano saa 6 usiku alikutwa akiiba debe moja la mpunga katika kijiji cha Fumagila Mashariki wilayani Nyamagana jijini Mwanza, akapigwa hadi kuuawa.


Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza,Valentino Mlowola, amesema watuhumiwa watano wa mauaji hayo wamekamatwa na amewataja kuwa ni William Mgemela(36) mwenyekiti wa Mtaa wa Fumagila Mashariki, Thomas Ndelembo(70), Makoye Majima(54),Mathias Masolwa(70) na Kachungwa Mshoni(57) ambaye ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Fumagila Magharibi.


Utafiti uliofanywa na mwandishi wa hari hii jijini Mwanza, unaonesha kuwa kwa muda mrefu sasa jijini humo kumekuwa na matukio ya watu kuwaua watuhumiwa wa makosa mbalimbali,kufuatia vyombo vya sheria kudaiwa kushindwa kutoa haki.


Katika tukio jingine watu wanaoshukiwa kuwa ni majambazi wamepora jumla ya shilingi milioni mbili na laki nne na simu za mkononi kwa wafanyabiashara wa M-Pesa huko Nyegezi Kona jijini Mwanza.


Washukiwa hao wakiwa na bunduki aina ya SMG walifyatua risasi majira ya saa 3 za usiku wa kuamkia leo na kuwapora simu na pesa Elionoga Antipas na Godfrey Christopher kisha kutoweka. Polisi wanaendelea na upelelezi wa tukio hilo.

Na Conges Mramba

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.