MTANGAZAJI

UTAFITI:MAKAMPUNI NCHINI TANZANIA YANAKWEPA KODI

Imebainika kuwa serikali ya Tanzania inapoteza mabilion ya shilingi kutokana na makampuni kukwepa kulipa kodi.

Kutokana na utafiti uliopo kwenye ripoti ya haki za binadamu na biashara ya mwaka 2013 iyotolewa jana jijini Dar-es-salaam na kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania unaonyesha kuwa kuanzia mwaka 2010 hadi 2012 makusanyo ya kodi yalikuwa ni asilimia 14 tu.


Utafiti huo umebaini kodi inachangia takribani asilimia 90 ya mapato ya ndani kwenye pato la taifa hilo ambapo katika kipindi cha miaka miwili kuna ongezeko la asilimia 4 tu kutokana na makusanyo ya kodi toka Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA).


Katika ripoti hiyo inaonyesha kuwa misamaha yakodi ilifikia zaidi ya shilingi bilioni mia sita ambayo ni asilimia 14.1 ya makadirio ya makusanyo na sehemu kubwa ya misamaha hii hutolewa kwa makampuni makubwa. Ambapo Tanzania hupoteza dola za kimarekani tirioni 1 kila mwaka katika mifumo mibovu ya fedha .

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.