KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU TANZANIA CHATOA MAFUNZO KWA WANAHABARI
Dk. Helen Kijo-Bisimba (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari kwenye mafunzo ya siku mbili ya waandishi wa habari kuhusu haki za wanawake kwenye Katiba, ushiriki wa vyombo vya habari kwenye mabaraza ya Katiba na haki ya kupata habari, kulia ni Mratibu wa Katiba wa kituo hicho, Anna Henga
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Helen Kijo-Bisimba amesema Katika Katiba mpya ni muhimu kuwekwa kipengere cha haki za wanawake ili kulisaidia kundi hilo.
Kauli hiyo aliitoa katika mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari kuhusu haki za wanawake kwenye Katiba, ushiriki wa vyombo vya habari kwenye mabaraza ya Katiba na haki ya kupata habari yaliyomalizika leo katika ofisi za kituo hicho kilichopo kijitonyama,Dar es Salaam.
Alisema katika Katiba ya sasa hakuna kipengere chochote kinachoelezea haki za wanawakwe mbali ya ibara ya 12 kutamka usawa wa binadamu.
Alisema kila mwanamke ana haki ya kuheshimiwa utu wake na kulindwa dhidi ya mila potofu na ubagunzi wa kijinsia.
Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika ambazo zimeridhia mikataba ya kimataifa mbalimbali ambazo zinawalinda wanawake kwa namna moja au nyingine.
Tafiti za kituo hicho zinaonesha kuwa kumekuwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia kama vilivyoainishwa kwenye Tamko la Umoja wa Mataifa la uondoaji wa Ukatili dhidi ya wanawake la mwaka 2005.
Ukatili huo ni kitendo chochote cha ukatili kuhusu jinsia, ambacho kinaweza kusababisha madhara, maumivu ama mateso ya kimwili au kisaikilojia kwa mwanamke, ikiwa ni pamoja na vitendo vya kutishia,kulazimisha, kunyima uhuru, bila kujali vimefanywa ama kwenye kadamnasi.
Mratibu wa Katiba wa Kituo hicho Anna Henga alisema ni wakati muafaka wa kuingiza kipengere hicho katika Katiba mpya tunayoitarajia kuipata.
Takwimu zilizotolewa katika mafunzo hayo zinaonesha kuwa kuna umuhimu wa nafasi za wabunge wa viti maalumu kwani wamefanikiwa kuchangia maswali ya nyongeza katika vikao vya bunge kwa asilimia 50 licha ya idadi yao kuwa chini ya 40.
Picha zote na Mwaibale blog
Post a Comment