MTANGAZAJI

HOSPITALI YA MUHIMBILI YAJA NA MBINU MPYA ZA MALIPO

 

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MABADILIKO YAMFUMO WA UKUSANYAJI MAPATO


Menejimenti ya Hospitali ya 
Taifa Muhimbili iko kwenye mchakato wa kutekeleza mikakati mbalimbali inayolengakuongeza mapato ili kuiongezea uwezo wa kifedha unaohitajikakatika kuboresha utekelezaji wa shughuli mbalimbali zaHospitali ikiwemo utoaji wa huduma kwa wagonjwa. Mikakati hiyo pamoja na malengo mengineyo, inakusudia kuhakikisha kuwa Hospitali inakusanya kikamilifu mapato yatokanayo naada mbalimbali wanazolipa wagonjwa ili kuchangia gharama za huduma mbalimbali zitolewazo hivyo kuongeza kiwango chaubora wa utoaji huduma ya tiba kwa wagonjwa.

Aidha, kufanikiwa kwa lengo hili kutaiwezesha Hospitali kuvuka lengo la kugharamia bajeti ya 
matumizi ya kawaida, kwa kutumia mapato ya ndani kwa asilimia arobaini kama Sera ya Mabadilikoya Taasisi za Umma inavyoelekeza. (Public Sector Reforms). Kwa sasa Hospitali inagharamia bajeti ya matumizi ya kawaidakwa kutumia mapato ya ndani kwa asilimia 58%.

Menejimenti ya Hospitali ya inategemea kuwa, mabadiliko haya ya mfumowa ukusanyaji wa mapato 
kwa kutumia benki, yataongeza makusanyo ya ndani kwa asilimia hamsini (50%) au zaidi na hivyo kuongeza uwezo wa kifedha wa Hospitali kugharamia bajeti ya matumizi ya kawaida kwa kutumia mapato ya ndanikutoka asilimia 58% hadi 72% katika mwaka wa fedha2013/2014.

Tunapenda kuwafahamisha 
kwamba moja ya mikakati inayotekelezwa na Menejimenti ya Hospitali ya Taifa Muhimbili, ni kuboresha udhibiti wa mfumo wa ukusanyaji mapato ya ndani.

Katika jitihada za kuboresha na kudhibiti mfumo wa ukusanyaji mapato unaotumika hivi sasa, 
Hospitali imeingia katika makubaliano na benki ya National Microfinance Bank (NMB) ambayo itatoa huduma ya ukusanyaji mapato kwa niaba ya Hospitali. Makubaliano ya kutoa huduma hii yalifikiwa baina ya Benki ya NMB na Hospitali ya Taifa Muhimbili mwezi wa Januari2013 na maandalizi ya kutoa huduma hii yalianza.

Maandalizi haya yapo katika hatua za mwisho na tunategemea kuanza kutumia mfumo mpya wa 
ukusanyaji mapato kupitiabenki ya NMB kuanzia siku ya Jumatatu, tarehe 11/03/2013.

Katika mfumo huu mpya wa kukusanya mapato, tutakuwa na vituo vitatu ndani ya 
Hospitali ambapo vituo viwili vitakuwa katika jengo la wagonjwa wa nje (New Outpatient Block) ambalo lipo mkabala na jengo la wazazi na kituo kingine kitakuwa katika jengo la kutolea huduma ya vipimo vya mionzi (lijulikanalo kama - Jengo la X-ray).

Katika mfumo huu mpya, mgonjwa atatakiwa kupata hati yagharama ya malipo ya huduma 
(bill note) itakayokuwa inatolewa na wafanyakazi wa Hospitali katika vituo ambavyo vitakuwa karibu na maeneo yote ya kutolea huduma. Hati ya gharama ya malipo ya huduma (bill note) itaonyesha huduma ambazo mgonjwa anahitajika kulipia na kiasi cha fedha zinazopaswa kulipwa. Baada ya kupata hati hiyo, mgonjwa ataelekezwa sehemu kilipo kituo cha benki ambako atafanya malipo na kisha kwenda sehemu ya kupata huduma inayohitajika.

Ili kuepusha usumbufu kwa wagonjwa, Menejimenti ya Hospitali imeandaa wafanyakazi maalum ambao watakuwa na mavazi maalum ili ( yaliyoandikwa niulize mimi) kuwaelekeza wagonjwa na wateja wetu wengine sehemu za kupata hati ya gharama ya malipo ya huduma 
na sehemu ya kulipia nakuwapa maelezo zaidi kuhusiana na utaratibu mpya wa malipo. Aidha, kutakuwepo na vibao vitakavyoelekeza sehemu vilipo vituo vya kulipia vya benki ya NMB.

Benki ya NMB itatoa huduma hii kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na nusu jioni, kwa siku za Jumatatu hadi Ijumaa. Siku za Jumamosi huduma ya malipo kupitia benki itatolewa kuanzia saa mbili na nusu 
hadi saa nane na nusu mchana. Muda wote ambapo vituo vya benki vitakuwa vimefungwa, huduma ya malipo itaendelea kutolewa kwa kutumia mfumo unaotumika hivi sasa katika kituo kimoja tu kilichoko Idara yaMagonjwa ya Dharura.

Ni mategemeo yetu kuwa wafanyakazi wote wa Hospitaliya Taifa Muhimbili pamoja na wateja wetu watatoa ushirikiano mkubwa na wa dhati ili kuiwezesha Hospitali kutimiza malengo yake ya kuboresha ukusanyaji 
mapato na hivyo kuongeza uwezo wa kifedha unaohitajika kuboresha huduma za matibabu,pamoja na kutimiza maelekezo ya Sera ya Uchangiaji wahuduma za afya.Ni matumaini yetu tutapata ushirikiano wa kutosha katikakutekeleza azma yetu.

Asanteni sana kunisikiliza.

Dkt. Marina Njelekela,
Mkurugenzi Mtendaji,
Februari 27, 2013.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.