MTANGAZAJI

TAARIFA YA TEF KUHUSU HALI ABSALOM KIBANDA
Picture
Rais Kikwete akimjulia hali Kibanda aliyelazwa katika hospitali ya Mill Park, Johannesburg, Afrika ya Kusini. Kulia ni Kinana. Rais Kikwete yupo Afrika Kusini kuhudhuria Mkutano wa Viongozi wa Vyama vilivyokuwa mstari wa Mbele kupambana dhidi ya Ukoloni na ubaguzi wa Rangi. Mkutano huo umeandaliwa na Chama cha African National Congress (ANC). (picha na Freddy Maro).


1. Kibanda leo ameingizwa theater ili kuanza kufanyiwa upasuaji na kujengwa sura baada ya kupungua kwa majeraha na uvimbe vilivyokuwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake, hususan kichwani na usoni.

2. Upasuaji huo unazingatia matokeo ya uchunguzi ulifanywa kwa zaidi ya saa 48 na jopo la madaktari na kubaini kwamba mbali na madhara ya awali, Kibanda pia aliumizwa taya lake la kushoto.


3. Kuhusu jicho lake la kushoto ambalo pia lilijeruhiwa, madaktari walisema wangetoa uamuzi kuhusu aina ya upasuaji ambao wangeufanya baada ya kubaini hali halisi wakati watakapokuwa wakijenga sura yake ambayo iliharibiwa kwa majeraha.


4. Wakati akipelekwa theater ambako alikuwa akifanyia upasuaji ambao uliotarajiwa kuchukua saa zaidi ya nne, alikuwa akilalamikia maumivu kutokana na kidonda kilichopo kwenye mguu wake wa kushoto. Kidonda hicho pia ni matokeo ya unyama aliyofayiwa.


5. Jana Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana ambao wako Afrika Kusini kikazi, walimtembelea Kibanda hosipitalini kumjulia hali. Rais Kikwete alisema Serikali inajitahidi kuwasaka wahusika wa tukio la utesaji wa Kibanda na kwamba wakikamatwa watafikishwa mahakamani.


Tutaendelea kufahamishana kila hatua ya tiba ya Mwenyekiti wetu, na tunaomba tuendelee kumwombea ili apone haraka.


-- 

Neville C. Meena,

Secretary General, 
Tanzania Editors Forum - TEF, Dar es Salaam - Tanzania.
Cell:
+255 - 787 - 675555 +255 - 753 - 555556
No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.