BIASHARA HARAMU YA WASICHANA KUTOKA TANZANIA KWENDA UARABUNI YASHAMIRI
Biashara ya binadamu imeibuka kwa
kasi nchini Tanzania na kutishia usalama wa nchi kutokana na watoto wenye umri
kati ya miaka 8-15 baadhi yao wakiwa wanafunzi wa shule za msingi na
sekondari kusafirishwa kinyemela kwenda katika nchi za kiarabu.
Uchunguzi wa kina uliofanywa na NIPASHE kwa takribani wiki mbili, umebaini kuwa biashara hiyo imeibuka kuanzia Desemba mwaka jana na imeshika kasi Januari mwaka huu na wanaosafirishwa wengi ni watoto wa kike kutoka mikoa mbalimbali nchini. Wapo wachache wa kiume pia.
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Maji, Mboje Kanga, alipoulizwa na NIPASHE alithibitisha kupata taarifa za kuwapo kwa biashara hiyo ingawa alisema kuwa hana takwimu za watoto ambao wamekamatwa wakitaka kusafirishwa.

“Tatizo la kusafirisha watoto lipo, lakini nina watu ambao
wanashughulikia suala hilo pale bandarini, nitafute kesho (leo) nitakupa
takwimu zote kuhusiana na biashara hiyo baada ya kuwasiliana na watu wangu.’’ Anasema
Kanga.
Taarifa zinaonyesha kuwa mawakala hao wakishafanikiwa kuwapata watoto hao kutoka katika mikoa hiyo huwapeleka Jijini Dar es Salaam na baadaye kusafirishwa kwa usafiri wa majini kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda Zanzibar.
Uchaunguzi umebaini kuwa watoto hao wakifikishwa Zanzibar hukutana na watu maalum ambao huwapokea na kufawanyia mipango ya kuwasafirisha kwa usafiri wa ndege au wa majini kwenda Uarabuni ambako hutumikishwa katika kazi mbalimbali.
Mawakala hao wakishafanikiwa kuwasafirisha kutoka Bandari ya Dar es Salaam, hulipwa wastani wa Dola za Marekani 5,000 (Sh. milioni 8) kwa kila mtoto wanayefanikisha kumvusha kutoka Tanzania Bara kwenda Zanzibar.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo, ili kuhalalisha safari za kuwasafirisha watoto hao, mawakala wanakula njama na baadhi ya wenyeviti wa serikali za mitaa kwa kuandika barua zinazoelezea sababu za watoto hao kwenda Zanzibar.
Barua hizo ambazo imebainika ni za kughushi, nyingi zinaandikwa na kupigwa mihuri ya wenyeviti wa serikali za mitaa wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, jijini Dar es Salaam.
Chanzo:wavuti
Post a Comment