MABANGO YA MORNING STAR TV YAGOMBANIWA
Timu
ya Morning Star Television imejikuta ikiingia katika wakati mgumu pale
umati mkubwa ulipowazunguka ukihitaji mabango ya MSTV. Hili limetokea
mara tu baada ya uhamasishaji juu ya kuchangia uanzishaji wa kituo hicho cha Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania, uliofanyika katika Kongamano la viongozi wa kanisa
Jijini Mwanza.
Wanasemina
wote wengi wakiwa ni wachungaji, watendakazi wa na wazee wa kanisa toka
South Nyanza Conference(SNC), Mara Conference , (MC) na Western
Tanzania Field(WTF) walipokea taarifa hii kwa furaha na kuahidi kutoa
ushirikiano katika kuhamasisha uchangiaji.
Kanisa hilo nchini Tanzania limeitenga March 2 ,2013 kuwa siku maalum
kuchangia TV ya kanisa itakayoanza juni 2013. Studio za Televisheni hiyo
ziko Mikocheni B,jijini Dar es salaam,ambapo mchakato wa uandaaji wa vipindi umeshaanza
Post a Comment