MTANGAZAJI

KUTOKA ARUSHA MJINI -MGOMO WA DALADALA NA BODABODA

 (Na Yona Maro-Arusha)

HALI YA ARUSHA MJINI KWA UJUMLA

Umeme hakuna maeneo mengi , umeme umekatika kama kawaida , kuna

makundi ya watu haswa wanafunzi walioshindwa kwenda mashuleni kutokana
na mgomo huu na wafanyakazi wengi wameenda makazini asubuhi wakati
mgomo bado haujaanza .

VIONGOZI WA MGOMO NA MALENGO

Mpaka sasa hakuna kiongozi wa mgomo huu aliyekuja wazi na kutoa sababu
za mgomo kwa umma hata wale waliogoma hawajui kwanini imekuwa hivyo .

KUATHIRIKA KWA UCHUMI

Uchumi unaweza kuathirika kutokana na watu kubadilisha ratiba zao za
kazi kutokana na mgomo huu lakini kwa kiasi kigodo sana mgomo wa
daladala arusha mjini hawezi kuwa na nguvu angalau kwa kipindi hichi .

KUHUSU MGOMO WA DALADALA


Wengi walianza mgomo baada ya kupeleka watu makazini na mgomo wenyewe

ulianzia kuanzia saa 2:30 , mimi nilikuwa nimeshafika maeneo ya
kilombero .

Hapa kuna vijana waliokuwa wanalazimisha wenzao wenye daladala

kusimama na kushusha abiria wote wasiendelee na safari yao ya mjini
kupeleka abiria kwahiyo walipaki hapo wale waliofikisha abiria mjini
hawakuweza kupakia abiria kupeleka maeneo mengine .

SABABU ZA MGOMO

Wengi wanatolea sababu ya kumuunga mkono mbunge wa Arusha Mjini kwa
kitendo cha kuwa rumande lakini hawajui ilikuwaje hawajui kwamba yeye
mwenyewe ndio aligoma dhamana na kwamba kuna taratibu za kumtoa
rumande alipokuwa na viongozi wa chadema mkoa wa Arusha wanaweza
kufanya hilo uwezo wanao .

KUHUSU BODABODA

Hawa wanaendelea kufanya kazi kwa asilimia kubwa na mpaka naanza
kuandika hili nimeona wamekuwa msaada mkubwa wa kupakia watu
kuwapeleka maeneo mbalimbali ya mjini wa arusha na pembeni .

KUHUSU BIASHARA MBALIMBALI

Biashara nyingi zinaendelea maduka mengi yamefunguliwa na wafanyakazi
wengi wameshafika makazini wanaendelea na shuguli zao za kawaida .

KUHUSU USALAMA WA RAIA NA MALI

Usalama ni mzuri na nimeona gari za FFU zikipita huku na kule katika
kuangalia usalama ila nimeona tukio moja maeneo ya stendi ambapo
baadhi ya vijana waliwazomea FFU hao na kutaka kuanza kurusha vitu
wakazuiwa na wenzao lakini usalama uko wa kutosha .

SIASA ZA CCM NA CHADEMA

Nilipokuwa stendi kuu ya arusha , kuna vijana walitishia kuwapiga kina
mama kwa tuhuma kwamba wao CCM kwahiyo hawapo kwenye mgomo huo na hizi
ndio siasa zinazoathiri kwa kiasi kikubwa mji huu kushindwa kufikia
baadhi ya malengo  yake .

TISHIO LA KUTISHIA KUVAMIWA KWA OCD WA ARUSHA

Wakati naendelea na shuguli zangu nilisikia habari za baadhi ya vijana
kutishia kumvamia OCD wa arusha kwa kuwa amewaita panya – Kama
mnavyokumbuka mara ya mwisho vijana hawa walivamia kituo cha polisi na
kusababisha mauaji mwanzoni mwa mwaka huu .

MKOA WA ARUSHA SIKU ZA MBELENI

Tukumbuke mkoa huu unategemea sana shuguli za utalii na maliasiri
kwahiyo hali hii ikiendelea kwa migomo na fujo nyingi shuguli za
utalii zitaadhirika kwa kiasi kikubwa vijana wengi watakosa ajira na
ajira nyingine zinaweza kufungwa kwa kukosa mitaji ya kuziendesha hili
ni jambo muhimu kwa vijana kuangalia .
Wengi wanaotishia migomo na hujuma mbalimbali ni ambao wako katika
viwango Fulani vya maisha kwa kiasi kikubwa hawaadhiriki na hali hii ,
wanaoadhirika ni wafanyakazi , wanafunzi wanoenda mashuleni na watu
wengine wasio nauwezo wanaotegemea huduma hizo .

VITA DHIDI YA UGAIDI

Kama tunavyojua ndugu zetu wakenya wanashiriki vita ya kuwaondoa
alshabaab nchini Somalia na nchi yetu kuunga mkono hatua hiyo kwahiyo
hata nchi yetu iko katika hatari ya mashambulizi ya kikundi hichi cha
kigaidi .
Tuwe makini makundi haya yanaweza kutumia migogo kama huu wa arusha
kutekeleza mauaji na hujuma zingine mbalimbali dhidi ya watanzania na
raia wengine wa nje
.
Lakini baadhi yetu wanaweza kuanza kufurahia na kushangilia tuwe
makini kwahili , tusivumilie vitendo hivi hata kidogo .

MSIMAMO WANGU

Nchi yetu inaendeshwa kwa sheria na taratibu ambazo ziko wazi na
hazijawahi kubagua wala kumtenga raia wowote kwa sababu yoyote ,
viongozi wawe mfano katika kutekeleza sheria na taratibu hizi na wawe
mifano kwa kutafasiri sheria hizi kwa wananchi wao haswa wale
waliowachagua au wale wanaowawakilisha sehemu mbalimbali nchini .

Nchi inavyoharibiwa kwa namna yoyote ile hata demokrasia ya kweli

hatutaweza kufanya na amani hatutakuwa nayo – nawaomba viongozi
wahakikishe wanalinda nchi hii pamoja na watu wake kama walivyoapa
pale bungeni na sehemu zingine walizokula viapo vya kulinda na kutetea
maslahi ya nchi .

 

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.