MTANGAZAJI

TANZANIA YATOA MSIMAMO WAKE KWA UINGEREZA KUHUSU USHOGA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Bernard Membe
Tanzania imetoa tamko la kukataa masharti ya Uingereza inayotaka nchi zinazotaka misaada yake ziruhusu vitendo vya ushoga.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alitoa msimamo huo leo Jijini Dar es Salaam akisema huko ni kwenda kinyume na sheria na utamaduni wa nchi yetu inayotambua ndoa ya mme na mke kama kiini cha familia.

Membe amesema hayo  alipokuwa akizungumzia mkutano wa Jumuia ya Madola uliofanyika wiki iliyopita huko  Perth, Australia.

Alitoa msimamo huo kufuatia kauli ya Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron kuwa wana mpango wa kusitisha misaada kwa nchi ambazo katiba na sheria zake hazitambui mashoga na ndoa zao.

  Amesema Tanzania inaheshimu sheria na utamaduni wake hivyo hatupo tayari nchi nyingine kutuwekea masharti kama hayo ya kuwa na uhusiano wa jinsi moja, hili ni tamko hatarishi linaloweza kuvunja uhusiano na nje.

Amesema tamko hilo ni msimamo wa chama cha Conservative na kibaya zaidi linatoka Uingereza ambako ndio wenye Jumuia ya Madola hivyo linaweza kusababisha kuvunjika kwa jumuia hiyo na ikitokea hivyo Uingereza ndio itakayowajibika

Miongoni mwa nchi 54 za Jumuia ya Madola kati yake nchi 13 ushoga ni sehemu ya katiba yao wakati 41 hazina utamaduni huo hivyo msimamo wa Tanzania ni kuwa na ndoa za jinsi mbili tofauti, kinyume na hapo unafungwa kifungo miaka 30.

Alisema kuendelea kukumbatia ushoga si jambo zuri na si la kulishabikia hata kidogo vinginevyo wanaweza kujuta nchi ikijihusisha na ushoga na kuukubali kupata misaada ya maendeleo.

Amesema Tanzania haiwezi kuyumbishwa kwa masharti ya kipuuzi bora tuitunze nchi yetu. Tanzania ni nchi maskini lakini kamwe haturuhusu kuingiliwa na nchi nyingine na kama ndo hivyo basi wakae na hela zao.
 
Tamko hili la Waziri Membe linakuja wakati watanzania wamekuwa wakitumia mijadala mbalimbali katika majukwaa na vyombo vya habari  kupinga  kauli ya Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron kuwa wana mpango wa kusitisha misaada kwa nchi ambazo katiba na sheria zake hazitambui mashoga na ndoa zao aliyoitoa wiki iliyopita kwenye mkutano wa jumuia ya Madola

1 comment

Anonymous said...

Lakini mbona balozi wa uingereza anasema sisi hatupo kwenye huo mkumbo kwa sababu tulishasign kitambo huo mkataba,huu utakuwa sasa ule msemo wa kiswahili,fumbo mfumbie mjinga.Kama ni kweli viongozi walishausign ni hatari sana kwa nchi na utamaduni pamoja na mila zetu zaidi na MUNGU wetu.

Mtazamo News . Powered by Blogger.