MTANGAZAJI

KENYA NA SOMALIA ZIMEOMBA MSAADA WA KIMATAIFA DHIDI YA AL-SHABAAB

Waziri Mkuu wa Somalia  Abdiweli Mohamed Ali (kushoto) na Waziri Mkuu wa Kenya  Raila Amollo Odinga wakionesha haki za makubaliano ya kupambana na al-Shabaab jijini  Nairobi Oktoba 31,2011.Picha na Reuters
Somalia  na  Kenya  zitafanya  mazungumzo  na wanadiplomasia  leo  mjini  Nairobi  kujaribu kuhamasisha  uungaji  mkono  kimataifa  kwa operesheni  inayoendelea  hivi  sasa   dhidi  ya kundi  la  Kiislamu  la  al-Shabaab.  Katika  taarifa ya  pamoja,  waziri  mkuu  wa  Kenya,  Raila Odinga na  mwenzake  kutoka  Somalia, Abdiweli Mohammed  Ali, wameomba  msaada  wa  kimataifa jana  kusaidia   ulinzi  katika  pwani  ya  Somalia  na bandari  ya  Kismayu, ambayo  wanaamini  ni  nguzo ya  kiuchumi  ya  kundi  hilo  la  al-Shabaab.


Ali  amesema  kuwa  serikali  ya  mpito  ya  Somalia inaiunga  mkono  Kenya , ambayo  imetuma  vikosi vyake  vya  jeshi   ndani  ya  mipaka  ya  Somalia mwezi  uliopita  kupambana  na  wapiganaji  wa  al-Shabaab, ambao  wanalalamikiwa  kuwa wanahusika  na  wimbi  la  utekaji  nyara na  mauaji.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.