KATIBU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI NCHINI TANZANIA ASIMAMISHWA KAZI
Habari zilizoifikia blog hii jioni ya leo toka Dodoma zinaeleza kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo (pichani) amesimamishwa kazi. Akiongea na waandishi wa habari mjini Dodoma mapema leo, Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, alisema kuwa Jairo amesimamishwa kazi kuanzia kesho ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili zilizotolewa bungeni mapema wiki hii.
Ilielezwa wiki hii bungeni kuwa Jairo anatuhumiwa kuandika barua ya kuchangisha fedha milioni 50 kwa idara 20 ili zitumike kushawishi wabunge wapitishe bajeti ya wizara yake. Haijaelezwa amesimamishwa kwa muda gani.
Post a Comment