MTANGAZAJI

KONDA NAYE AJA NA KIKOMBE

 

MKAZI wa Mbagala jijini Dar es Salaam, ameibuka na kusema kuwa ameoteshwa na Mungu kutoa dawa kwa njia ya kikombe kutibia wagonjwa wenye maradhi sugu.
  Dawa hiyo amedai Mungu amemuotesha kutoa dawa ambayo ni maji ya kisima, bomba na haichanganywi na chochote zaidi ya maji hayo.

Awali kijana huyo aliyekuwa akiabudu dini ya Ukristo na baadae kubadili dini na kuwa Muislam na ndipo ameoteshwa.


Awali imedaiwa kijana huyo alikuwa akifanya kazi ya ukonda katika daladala na hivi karibuni ameibuka na kudai kuwa ameoteshwa.


Kufuatia taarifa hiyo watu wameanza kujitokeza nyumbani kwa kijana huyo kupata kikombe cha dawa hiyo huku akiwa ameshika msaahafu mkononi.


Hata hivyo Kamanda wa Polisi Temeke, wanafanya jitihada za kufanya mahojiano maalum na kijana huyo na taarifa itatolewa kwenye vyombo vya habari.


Kijana huyu ni wa saba kujitokeza na kudai wameoteshwa na Mungu na wengine wamejitokeza katika mkoa wa Mbeya, Moshi, Mbeya, Iringa, Tabora na Morogoro, Pwani wote wakidai kuoteshwa na Mungu kutoa tiba kwa njia ya kikombe.
Kutoka:NIFAHAMISHE

2 comments

Anonymous said...

Read Mathew 24:24-25, Mathew 7:15-20,1John 4:1-3, Isaiah 8:20 and many more. A lot more of these crooks and quakes will come and go, saying they have been sent by God. If they go by what those verse say, well and good. If they don't well,do what you have to do. As for me I will punch them in the face because I hate liars. (if i offend someone by the actions i might take,sorry. but that's my personal opinion) Benj

mwalimu said...

Na bado wataongezeka yaani kwa sasa tunazungumzia kimkoa itafikia sasa kila kitongoji,kila dini,kila ukoo utakuwa na mwakilishi aliyeoteshwa.Hata wale ambao hawana ajira wataona sehemu ya kupata fedha ni kudai wameoteshwa maana ndo watu wataamini kwa haraka zaidi

Mtazamo News . Powered by Blogger.