MTANGAZAJI

WANAOTUHUMIWA KUTAKA KUMUUA DK. CHEGENI KIZIMBANI


WATU wanne wanaotuhumiwa kwa kula njama za za kutaka kumuua Aliyekuwa mbunge wa Busega Dk. Raphael Chegeni wamefikishwa kizimbani  na kusomewa shitaka linaloakabili.

Washitakiwa ambao wamefikishwa mahakamani mbele ya hakimu mkazi mfawidhi Angelous Rumisha, ni Ellen Joseph Bogohe (54) ambaye ni mshitakiwa wa nne, ni Dismas Zacharia Ndaki (47), Erasto Kazimili (48), Queen Joseph Bogohe (37) wote kwa pamoja wakikabiliwa na shitaka moja ambalo inadaiwa walilitenda kati ya Februari 11 hadi Aprili 13 mwaka huu.

Washitakiwa namba moja na mbili ambao ni Dismas na Erasto walikuwa wakitetewa na wakili Benard Kabonde huku washitakiwa anmba tatu na nne ambao ni Ellen na Queen walikuwa wakitetewa na Mathew Nkanda na Laurian Vedastus.

Mara bada ya shauri hilo kuanza majira ya saa 9: 24 alasiri, hakimu alianza kujadiliana na mawakili wa pnde zote za utetezi na serikali na iwapo shauri hilo linapaswa kusikilizwa na mahakama hiyo au mahakama kuu.
Mvutano huo ulihitimishwa na hakimu huyo baada ya kukubaliana kuhairisha kesi hiyo hadi kesho (leo) ili kufuatilia kwa kina sheria iwapo shauri hilo linaweza kusikilizwa na mahakama hiyo au makama kuu.
Kutokana na uamuzi huo ulianza mvutano kuhusiana na dhamana kwa watuhumiwa huku wakili wa utetezi Kabonde aliomba mahakama hiyo kuwapatia zamana washitakiwa wote kwa hadi leo ambapo kesi hiyo itakaposikilizwa.

Ombi hilo lilipingwa na wakili wa serikali Marungu ambaye alisema kwa vile uhalifu wao unahusisha mtandao (Cyber Crime) washitakiwa wanaweza kuingilia na kuvuluga upelelezi wa kesi hiyo hivyo kuomba mahakama kuwanyima dhama.

Hoja hiyo ilipingwa na wakili wa utetezi na kudai kuwa watuhumiwa walistahili dhamana kwa vile tayari wakiwa mikononi mwa Polisi wanaoshuhgulika na uchunguzi walipewa dhamana.

Hakimu Rumisha akitoa uamuzi wake alisema kuwa kwa vile muda wa mwisho mahakamani ni saa 9: 30 na wakati huo ilikuwa ni saa 9: 59 alisema washitakiwa watakwenda rumande hadi leo majira ya saa 5:00 ambapo shauri lao litafikishwa kwake na kutolewa maamuzi iwapo linapaswa kusikilizwa na mahakama yake ama laa.

Na Frederick M. Katulanda

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.