KONDA NAYE AJA NA KIKOMBE
MKAZI wa Mbagala jijini Dar es Salaam, ameibuka na kusema kuwa ameoteshwa na Mungu kutoa dawa kwa njia ya kikombe kutibia wagonjwa wenye maradhi sugu.
Dawa hiyo amedai Mungu amemuotesha kutoa dawa ambayo ni maji ya kisima, bomba na haichanganywi na chochote zaidi ya maji hayo.
Awali kijana huyo aliyekuwa akiabudu dini ya Ukristo na baadae kubadili dini na kuwa Muislam na ndipo ameoteshwa.
Awali imedaiwa kijana huyo alikuwa akifanya kazi ya ukonda katika daladala na hivi karibuni ameibuka na kudai kuwa ameoteshwa.
Kufuatia taarifa hiyo watu wameanza kujitokeza nyumbani kwa kijana huyo kupata kikombe cha dawa hiyo huku akiwa ameshika msaahafu mkononi.
Hata hivyo Kamanda wa Polisi Temeke, wanafanya jitihada za kufanya mahojiano maalum na kijana huyo na taarifa itatolewa kwenye vyombo vya habari.
Kijana huyu ni wa saba kujitokeza na kudai wameoteshwa na Mungu na wengine wamejitokeza katika mkoa wa Mbeya, Moshi, Mbeya, Iringa, Tabora na Morogoro, Pwani wote wakidai kuoteshwa na Mungu kutoa tiba kwa njia ya kikombe.
Kutoka:NIFAHAMISHE
Post a Comment