MTANGAZAJI

MORNING STAR RADIO 105.3 FM SASA KWENYE HOPE CHANNEL INTERNATIONAL

Mtangazaji akiwajibika ndani ya Morning Star Radio

Yusufu Mcharia mmoja wa watangazaji wa Morning Star Radio 105.3 fm


Sasa unaweza kusikiliza matangazo ya Morning Star Radio 105.3 kwa lugha ya kiswahili kupitia satelite katika Hope Channel International,ili kuyapata matangazo yetu inakupasa uwe na Satelite Dish na kulitune katika C-BAND na kuingia katika Satelite ya THAIKOM ndipo utaweza kuipata Hope Channel na utaingia katika channel namba nne ya audio ndipo utaipa Morning Star Radio inayomilikiwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania ikirusha matangazo yake toka Mikocheni B jijini Dar es salaam

12 comments

Mr. MHOJA said...

Je, Radio yenu haipatikani Mtandaoni? Sisi tulioko nje ya Tanzania wengi tunatumia kusikiliza redio kupitia mitandaoni tu.

Hatutumii "dishes", zinachafua sura za majengo. Katika nchi zisizokuwa na "Cable Channels" ndiko wanakotumia zaidi dishes, mostly nchi maskini.

Radio Maria Tanzania, tunaipata vizuri sana kupitia mtandaoni. Tungependa na ninyi tuwapate.

Mr. MHOJA

fredmlay said...

Changamkeni hapo mikocheni, maendeleo ni mtandao zaidi sio dish, wekeni vipindi live kwenye net.

kwakifupi wasabato tumezubaa, tulipaswa hata kuwa na mikataba na startimes ili hope ionekane kitaifa kupitia tbc/startimes.

muda ndio huu kabla wapinzani wetu hawajatufungia milango na madirisha.

mwijarubi shida said...

Tunahitaji pia nyimbo za zamani za kwaya kama vile kurasini na zingine nyingi,tudownload and then injili isonge mbele

emmanuel tang'ale said...

BRO EMMANUEL TANG'ALE

JAMANI EBU WAADVENTISTA WOTE TUAMKE HII RADIO SIO ISIKIKE DAR TU EBU TUFANYE MAPINDUZI MAKUBWA ILI ISIKIKE TANZANIA NZIMA NA NJE YA NCHI KWA NJIA YA INTERNET KWANI NI RADIO AMBAYO IMEPANGILIWA VIPINDI VYAKE LAKINI TUNAZIDIWA NA VIKANISA VIDOGO SANA SIE TUKO PALEPALE JAMANI KUMEKUCHA TUFANYE KAZI.

Felix Mbekenga said...

thnx morning star radio! kwa kazi mnayoifanya nzuri!

Anonymous said...

bwana yesu asifiwe
naomba sana mwongozo wa kujifunza biblia uwabadilishe mwenyekiti DJ maregesi na elizabeth Nyang'ura sababu wanakwaza sio katika radio lakini wanasabaisha roho kupotea

Nyagabona Daudi Ngalya said...

Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayofanya ya injili, kwani ni watu wengi sana wamekutana na Yesu kupitia huduma yenu nzuri.

Nimekutana na shuhuda nyingi sana za watu wanaoingia kanisani si kwa injili nyingine bali kupitia vipindi vya radio hii.

Mungu mnayemtumikia hatanyamaza kimya kama mkiendelea kuwa waaminifu kwake na kuishi sawasawa na neno lake.

Nyagabona D Ngalya

Anonymous said...

BWANA YESU ASIFIWE SANA KWANI SASA RADIO YETU YA MORNING STAR INASIKIKA TARIME;TUNAENDELEA KUFURAHIA MATANGAZO;MATANGAZO YATOLEWE MAKANISANI ILI WATU WAWE NA TAARIFA: WENU KTK BWANA KENEDY SIMION WERE

Haule Computer & Phones Repair said...

Bwana Yesu asifiwe
Kwakweli mimi na familia yangu tunabalikiwa sana na vipindi vya redio morning star hasa lulu za injili na vipindi vya mahubili jinsi mnavyofungua ukweli bila kuficha, Mungu awabaliki na neema ya bwana wetu Yesu kristo iwe pamoja nanyi nyote..

Mihayo Sizya said...

Mimi nawapongeza sana kwa Kazi kubwa na Ngumu mnayoendelea kuifanya MUNGU na awabariki na Awapatie maarifa zaidi na zaidi kundeleza mbali Duniani kote Kwa Neema yake Ushauri wangu sisi Washiriki tunayo nafasi ya kusapoti kwa kadri tuwezavyo mawazo na michango yetu ya hali na mali ili injiri izidi kusonga mbele Bwana Na awabariki sna wote Mtakao soma huu ujumbe.

pharesdamian said...

Katika lulu za injili,kwanini sijasikia wimbo wa ambassador Rwanda unaozungumzia sabato?

Unknown said...

God be with u when u are working and witnessing his love

Mtazamo News . Powered by Blogger.