MTANGAZAJI

WADAU WA MCHEZO WA NGUMI ACHENI USANII

Kitendo cha Rais wa PST Emanuel Mlundwa kuwatangazia mashabiki wa ngumi kuwa bondia toka Argentina Enrico Areco aliyepaswa kupigana na Bingwa wa mkanda wa ICB na WBO,uzito wa Bantamu Francis Cheka toka Morogoro Desemba 19 mwaka huu kuwa hakufika kutokana na uzee ninakiita ni kichekesho,usanii na ubabaisha katika mchezo huo!!.

Kiongozi huyo ambaye aliwatangazia mashabiki wa mchezo huo kuwa Areco hakufika nchini dakika chache kabla ya kuanza mpambano huo kwenye ukumbi wa PTA,Sabasaba na kuwaambia kuwa wamebadilisha bondia na kumleta bondia Isak Tawares toka Brazil na kusababisha kuzomewa na mashabiki hao.

Swali ni kwamba Je PST na TPBC hawakufahamu kweli kuwa Enrico Areco alizaliwa mwaka 1964 toka mwanzo wakati wanaanza mikakati ya pambano hilo jambo ambalo haliingii akilini katika ulimwengu huu ambao dunia ni kijiji kimoja ambapo kupitia wavuti huwezi kutumia hata dakika moja kufahamu historia fupi ya bondia huyo toka Argentina.

Nakumbuka siku tatu kabla ya pambano hilo redio moja maarufu jijini Dar es salaam ilimkariri mmoja wa waandaaji wa mpambano huo akisema wameshatuma tiketi Argentina na mambo yote yako sawa.

Blog hii imejaribu kuwasiliana na Cheka kuhusiana na suala hili lakini hajaweza kuzungumza lolote.

Wakizungumza na waandishi wa habari jana wadau wa mchezo huo Japhet Kaseba ambaye ni bingwa wa dunia wa kick-boxing na Ali Matumla mzazi wa mabondia hapa nchini wamesema suala hili linamdidimiza mchezo huo hapa nchini

Katika mpambano huo Cheka alimpiga kwa knock-out katika raundi ya pili bondia Isak Tavares toka Brazil na kutetea mikanda yake.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.