TIMU YA WATOTO WA MITAANI TANZANIA KUSHIKI KOMBE LA DUNIA
Timu ya soka ya watoto waishio kwenye mazingira magumu(mitaani) ya jijini Mwanza, Tanzania ni miongoni mwa timu 9 duniani zitazoshiriki kombe la dunia la watoto wa mitaani mashindano yatakayofanyika March 2010 kwa mara ya kwanza Durban, Afrika ya Kusini.
Timu hizo ambazo zitawakutanisha watoto wa mitaani ikiwa ni njia ya kueleza matatizo yao kupitia katika mchezo wa soka unaopendwa na watoto duniani zinatoka katika nchi za Tanzania,Brazil,India,Nicaragua,Phillipines,Ukraine,Vietnam,Afrika ya Kusini na Uingereza .
Timu toka Tanzania inashiriki mashindano hayo kutokana na juhudi binafsi za Mwalimu Mutani ambaye pia amefanikiwa kuishawishi klabu ya Arsenal ya Uingereza katika kusaidia maendeleo ya timu hiyo ya kituo cha Caretakers ya jijini Mwanza
Post a Comment