MTANGAZAJI

RAIA WA KOREA KUKIUKA SHERIA

Kwanza niwatakie wote Heri ya Krismass na Mwaka Mpya 2010, halafunichukue nafasi hii kumpongeza Bw. Jerry Muro kwa kipindi chakeanachokiendesha pale TBC1 pia nimpe pole kwa kitendo cha udhalilishajialichofanyiwa na yule mwanamke fedhuli wa kicanada.

Nikurudi kwenye mada husika, ni kwamba nimefuatilia kipindi cha usikuwa habari kilichorushwa kwa siku mbili mfululizo yaani Jumanne 22Disemba 2009 na Jumatano 23 Disemba 2009.

Katika kipindi hiki Bw.Jerry Muro na timu ya TBC1 walirusha sakata la raia wa Korea aitwae AnSu Jing alieingia nchini kwa kofia ya umishonari akitaka kuubiri nenola mungu jijini Dressalaam, lakini kwa karibu miaka kumi sasa amekiukataratibu za nchi na kuamua kuhama Dar na kuhamia Bagamoyo na kuanzishashughuli za kilimo pamoja na kuendesha kampuni ya uchimbaji udongo wamadini ya kauli, huku akijenga kanisa dogo kuendesha shughuli za
kichungaji. Kwa bahati mbaya katika kuendesha shughuli zake hizoamekuwa akiwanyanyasa wafanyakazi wake ambao ni ndugu zetu waliotokasehemu mbalimbali za nchi yetu hadi kufikia kuwatukana na kuwapiga.Vile vile amekuwa akiwakata mishahara yao kwa asilimia kumi akidai nikulipa fungu lakumi katika kanisa lake.


Cha kushangaza Bw. Muro katika kufuatilia swala hili ilibainika kuwahakuna ofisa yoyote wa wilaya ya Bagamoyo anehusika na ardhi auuhamiaji alionyesha kufahamu lolote kuhusu mchungaji huyo Mkoreakuendesha shughuli zake pale na jinsi alivyopata uhalali wa kumilikiekari zaidi ya 50.

Lakini baada ya kipindi hiki kurushwa hewani na Mh. Abdi Ijimbo(kutoka uhamiaji) kujikanyaga katika kujibu maswali ya Bw. Muro sikuiliyofuata idara ya uhamiaji Bagamoyo ilimfikisha mahakamani Mkoreahuyo na mke wake kwa makosa manne.

1. Kukiuka sheria za uhamiaji kwakuhama Dar kwenda Bagamoyo bila ruhusa kwavile kibali chake kilimtakaawepo Dar na si penginepo.

2. Kuendesha biashara ambazo hakuziombeakibali alipoingia nchini.

3. Kumsaidia mkewe na mtoto wake kufanyakazi nchini wakati kibali kinaonyesha wao ni wafuasi wake katikakanisa lake.

4. Kufanya ajira kinyume na sheria za ajira za Tanzania.

Nimelazimika kutoa maelezo hayo machache hapo juu ili kwa wale ambao kwasababu moja ama nyingine hawakubahatika kukionakipindi hicho wapate mwanga wa kuijadiri hoja hii, ambayo msingi wakemkubwa ni swali hapo juu kwamba je ni kweli wahusika (uhamiaji naardhi) hawakuwa na taarifa na mkorea huyo kwa miaka yote kumialiyovunja sheria za nchi? Pia si vibaya tukitoa na mapendekezo yanini kifanyike kuwafichua wengine ambao naamini wapo wengi wa ainahiyo hapa nchini.

EMMANUELEY P. MGONGO
emmanueley@iwayafrica.com
www.wanabidii.net

1 comment

Mzee wa Changamoto said...

Kaka MADUHU
Kwa niaba ya familia yangu na wapenda mema wote nakutakia kila lililo jema wakati huu wa sikukuu na usalama kuelekea mwaka mpya
Baraka kwako

Mtazamo News . Powered by Blogger.