MTANGAZAJI

UTAMADUNI WA KUSOMA/KUJISOMEA

Siku chache zilizopita nilikuwa na kasafari ka kwenda mkoani morogorokwenye basi nililopanda mimi mwenyewe ndio nilikuwa na gazeti lakusoma nakumbuka nilikuwa nasoma gazeti la mwanahalisi , kwenye basihakukuwa na mtu aliyeshika kitabu cha kusoma wala gazeti wala jaridalolote sembuse yule ambaye anasikiliza radio za nyumbani kusikilizayanayojiri .

Nyakazi za asubuhi zile wakati wa mchaka mchaka wa makazini namashuleni ingia kwenye daladala uone wanafunzi ukiona ameshika kitucha kusoma basi ujue ana mtihani baadaye ana kariri cha kwenda kujibukwenye mtihani huo kama hakuna mtihani utafikiri hata sio mwanafunzihata shuleni anachelewa kwa dakika chache .

Ukipita vyuoni napo ndio utashangaa zaidi ukienda kwenye internetcafé angalia history ya search ujue wanafunzi walikuwa wana searchnini au kuangalia aina ya tovuti walizokuwa wanatembelea utashangaa nakustaajabu mfano wa UDSM samahani kwa sasa hakuna huduma ya internetcafé kwa miezi 2 sasa ila ni asilimia chini ya 10 ya wanafunziwanaotembelea tovuti hiyo kwa siku kwa ajili ya kazi za kila siku hapovyuoni .

Ukitembelea stationary zao kuangalia kwa mfano kinachoandikwautashangaa mfano watu 20 wameandika jibu moja kwenye swaliwaliloulizwa si inaonekana kwenye print out pale tofauti ni majina yawanafunzi tu ingawa hii zaidi inatokea kwenye taarifa za field.

Hii ni tofauti sana na Nairobi au mombasa ambapo huwa naenda mara kwamara kule watu wanapenda kusoma kuanzia wanafunzi mpaka wafanyakazipamoja wadau wengine wa masuala ya nchi yao .

Hata unapoingia kwa mfano kwenye forum za nchi jirani utaona nakuamini watu wengi wanapenda kusoma na kuandika tofauti ya nyumbanikwetu kwa mbali kidogo nimeona hili kwa sababu nimetunga riwaya kadhaazimesomwa sana na watu wa huko mpaka sasa hivi naendelea kuandaa fupifupi .

Naona zifanyike jitihada za dhati kabisa kuamsha utamaduni wa kusomakwa watanzania wote hii ni pamoja na wadau wa kuandika na utunzi kukaapamoja kufanya utafiti na kujua kitu hichi kifanywaje ili hali iwenzuri .

Mfano kwa mimi nimegundua wengi wanapenda vitu vifupi fupi ilaukimwandikia mwanamke wa kikuyu kitu kifupi ataomba uendelezeekuandika mpaka umalizie yote uliyotaka kusema .

Yona F Maro

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.