MTANGAZAJI

TANZANIA @ 48


Ndugu zangu tarehe 9 Mwezi ujao nchi yetu itakuwa inatimiza miaka 48 toka kupata uhuru wake , Toka wakati huo kuna mengi sana yamefanyika kutokana na mipango ambayo ilikwepo wakati huo hata mengi pia ambayo hayakufanyika kwa sababu mbalimbali .
Tungependa kuwa na mjumuiko mwingine wa wanabidii ambao utakutanisha watu mbalimbali waliokwepo wakati huo na mpaka sasa hivi Tungependa kujadili vitu mbalimbali kwenye mjumuiko huo wa wanabidii ambao kwa jina ni TANZANIA @ 48
Kabla ya mjumuiko huo tunaweza kushiriki mjadala huo hapa hapa kwenye mtandao kama huwezi kushiriki kwa kuandika tuma picha na maelezo mengine ambayo unafikiri yanaweza kuleta changamoto kwa kizazi hichi
KARIBUNI SANA
Yona Fares Maro

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.