MTANGAZAJI

ATM ZINAPOKUWA KEROHivi hizi ATM zilizowekwa katika mabenki ni mchezo wa kuigiza ama ni nini hasa?Mfano hapa Morogoro toka Alhamisi iliyopita ATM za bank ya NBC zilikuwa hazifanyi kazi hii si mara ya kwanza ni mara nyingi tu na si tatizo hili linatokea unaenda kuchukua pesa yako kwa ajili ya matumizi unakuta mstari mrefu ama haifanyi kazi si NBC tu hata NMB.

Mfano hapa Morogoro kuna ATM zisizopungua tano za bank ya NBC cha kushangaza ni kwamba unaweza kuta zote hazifanyi kazi,kilichonikera zaidi siku ya alhamisi ATM palepale bank ilikuwa haifanyi kazi na ndani ya bank walikuwa wanapokea pesa tu na si kuchukua pesa,sasa pesa za wananchi ,ambazo hata hizi kazi zetu za kipato cha chini tunaambiwa kupokelea banki inakuwaje???

Nilishangaa kukuta wafanyakazi wa kampuni moja ya Tumbaku wakiwawamesubiri mshahara wao wa siku 15 toka asubuhi na mimi nilifika hapo saa 10 jioni.

Ninavyofahamu kuna watu wa IT katika mabenki yetu na wamepewa majukumu ya kuhakikisha ATM zinafanya kazi na wanalipwa pesa nyingi je wako makini na kazi yao kweli??? na Je hizi ATM ziko katika ubora unatakiwa kweli ama ni danganya toto????

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.