MTANGAZAJI

RAIS JAKAYA KIKWETE KUZUNGUMZA LIVE NA WANANCHI LEO

Watanzania tutamwuliza na kumshauri nini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete?? Hili ni swali ambalo majibu yake nayasubiri kwa hamu kubwa siku ya leo ambapo kiongozi huyu wa awamu ya nne hapa nchini atakapozungumza moja kwa moja na wananchi kupitia Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) kuanzia saa mbili na nusu usiku.

Vituo vingine vitakavyoonesha mazungumzo hayo ambayo rais atatumia nafasi hii kusikiliza hoja,ushauri na kujibu maswali ni Tumaini TV,TVZ,ITV,Channel Ten na TV Mlimani.

Namba za simu zitakazotumika kwenye mazungumzo hayo ya moja kwa moja na kusikika pia kupitia redio za Clouds FM,Sauti ya Tanzania Zanzibar,Radio Tumaini,Radio Uhuru,Radio Mlimani na TBC-Taifa ni:
+255 -22-2772448
+255-22-2772452
+255-22-2772454
Ujumbe mfupi wa maneno (SMS)unaweza kutumwa kupitia nambari:
+255 788 500019
+255 764 807683
+255 714 591589
Hali kadharika waweza kutumia anuani ya barua pepe ambayo ni swalikwarais@yahoo.com

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.