MTANGAZAJI

MASHINE ZA ATM ZA NBC ZAFUNGWA KWA SIKU MBILI

Katika mojawapo ya magazeti ya kila siku hapa nchini toleo la jana kulikuwa na tangazo la Benki ya Taifa ya Biashara kufunga ATM mashine zake nchi nzima kwa muda wa siku mbili leo na kesho.

Baada ya kuona tangazo lile nilishindwa kuelewa japo sababu ilikuwa ni kuboresha mashine hizo Duuuu!!! KAZI IPO!!! Kwanza nilijiuliza kwamba hivi ni watanzania wote wanaosoma gazeti lile?? hivyo si watanzania wote wanaoweza kulisoma gazeti lile kutokana na utamaduni wa watanzania wengi kutopenda kusoma hili nalo ni tatizo.

Pili katika hali hii ya utandawazi na teknohama inavyobadilika hivi hakuna njia yoyote ambayo inaweza kutumika kutatua tatizo hili pasipo kuzifunga mashine hizi na waliopewa jukumu hili katika benki hii kubwa hapa nchini hawawezi kutafuta njia mbadala???????????muda mfupi uliopita mama mmoja anashangaa kusikia toka kwangu kuwa mashine hizo zimefungwa kwa siku mbili.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.