MSAMAHA WA KODI-SERIKALI YATOA TAMKO
Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda
Serikali ya Tanzania imebatilisha uamuzi wake wa kufuta msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani(VAT) kwa taasisi za dini na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGOs) na kuunda Timu Maalum itakayofutilia mianya ya matumizi mabaya ya msamaha huo.
Akitangaza uamuzi huo jana Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema Serikali italazimika kurekebisha vipengele kadhaa kwenye bajeti ya sh. bilioni 9.5 iliyosomwa wiki iliyopita bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Mustafa Mkulo na kuweka vipya kwa baadhi ya maeneo ili kukidhi marekebisho hayo.
Waziri Mkuu baada ya Serikali kusikia kilio cha wabunge na taasisi za dini, alikukutana na viongozi dini juzi na kukubaliana kwamba ni umuhimu wa kuendeleza msamaha huo kwa sasa huku wakimwahidi kushirikiana na Serikali kudhibiti matumizi mabaya ya misamaha hiyo.
Pinda alieleza kuwa Wabunge hasa wa CCM walipigia kelele suala hili na kuishauri Serikali kuangaliaupya. Viongozi wa dini nao walisema hivyo, ile rai ilikuwa ya msingi, jana (juzi) nilipata fursa ya kukutana na viongozi wa dini maaskofu, alikuwepo Askofu Mokiwa (Valentino-Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania), Malasusa(Alex Askofu Mkuu wa Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania -KKKT), Rwaichi (Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Kanisa Katoliki), Katibu Mkuu wa Kanisa Anglikan Tanzania,(Dkt. Raphael Mwita), Shekhe wa Mkoa na mashekhe wengine.
Tangu kutolewa kwa bajeti ya mwaka 2009/10 Viongozi wa dini wamekuwa wakiisihi sana Serikali iangalie upya jambo hili, kwa kueleza kuwa kazi zao wanasaidiwa na wahisani wa nje wanaojinyima na kwa kufanya hivyo inaweza kuwavunjamoyo na kuwa na athari kubwa kwetu Tanzania.
Akizungumza na TBC1 jana usiku Askofu Mkuu Msaidizi jimbo la Dar es salaam,Methodius Kilaini alisema amefurahishwa na uamuzi wa serikali na alijuwa kuwa serikali itabadilisha maamuzi hayo kwani maamuzi kama hayo yalishawahi kutolewa na awamu za uongozi uliopita nchini Tanzania.
Hata hivyo watafiti wa mambo wanaeleza kuwa kuna baadhi ya watendaji wa mashirika yasiyo ya kiserikali na taasis mbalimbali za dini nchini wamekuwa wakitumia fulsa ya kusamehewa kodi na kujinufaisha wao binafsi na familia zao
Post a Comment