MTANGAZAJI

VIPAJI VIPO-MIKAKATI HAKUNA




Ukiwauliza wanasoka nyota unaowafahamu wewe hapa duniani watakueleza jinsi walivyokumbana na changamoto tangu wakiwa wadogo hadi kufikia mafanikio waliyonayo sasa.
Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi nyingi barani Africa ina vijana wengi walio na vipaji vya mchezo wa soka ulio na mashabiki wengi duniani,lakini ni nani ambaye "atajitoa mhanga" kwa ajili ya vijana hawa.
Maana miundo mbinu ya kuwasaidia kufikia kile ambacho sasa wanakiona kwa kupitia luninga inaendelea kumilikiwa na wajanja wachache wakiweka vitega uchumi kwa ajili ya matumbo yao na familia zao.
Angalia vijana hawa hawana vifaa vya michezo uwanja wenyewe wanaufyeka wenyewe hakuna wa kuwasaidia je tutatoka kweli kwa mtindo huu? ama tutaendelea tu kushangilia picha kwenye luninga??? Mi naamini Tanzania na Africa kwa ujumla kuna kina ETO wa kumwaga lakini ubinafsi na kujipenda nafsi kwa waafrika na viongozi wetu ndo kunakotufanya tusifikie kwenye kilele cha maendeleo.sijui tutabadilika lini na nani aliyetuloga????


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.