MTANGAZAJI

TAIFA STARS WAKIAMUA WANAWEZA!!!

Kikosi cha Taifa Stars jana (picha toka Michuzi blog)

Jana usiku timu ya soka ya Taifa,Taifa Stars ilitupa Watanzania kile roho inapenda katika mchezo wa soka wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja mpya wa Taifa kwa kuifunga timu ya soka ya New Zealand bao 2-1.

Bao la kwanza la Taifa Stars lilifungwa na Jerry Tegete aliyesawazisha baada ya kuwa tumefungwa bao na wageni kwa njia ya tuta.Bao safi la pili na ambalo linaingia katika mojawapo ya mabao safi yaliyofungwa kwenye uwanja mpya na timu ya Taifa lilifungwa na Mwinyi Kazimoto dakika chache kabla ya mechi kumalizika.

Wadau wa soka wanapendekeza kuwa kikosi cha Taifa Stars kisibadilikebadilike ili kujenga timu imara.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.