MTANGAZAJI

WEST HAM UNITED NA MRISHO NGASA

Nimekuwa nikifuatilia suala la majaribio ya mchezaji wa Yanga na Timu yetu ya Taifa(Taifa Stars) Mrisho Ngasa(Jezi namba 8 pichani juu) tangu aondoke kwenda kufanya majaribio huko Uingereza .

Ninachosikitika ni jinsi suala la Ngasa linavyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari hapa Tanzania,nashindwa kuelewa waandishi wa habari za michezo hapa Tanzania wanashindwa kupata habari za uhakika kuhusu Ngasa kweli ni uzembe,kutojali ama ni nini?

Jumapili iliyopita baada ya mechi ya Simba na Yanga nilikuwa nyumbani kwa mmoja wa kiongozi mwandamizi wa bank ya NMB ambaye aliongea na Ngasa kwa simu moja kwa moja toka Uingereza kuhusu maendeleo ya majaribio katika Club cha West Ham na mazungumzo yale niliyasikia ambapo Ngasa alisema kuwa ameongezewa muda wa kufanya mazoezi hadi ijumaa ya wiki hii na akaeleza kuwa kwa mtazamo wake ananafasi ya kufanya vyema.Pia katika mazungumzo yale Kiongozi huyo alitoa pendekezo kwa Ngasa kuwa kama imeshindikana West Ham ajaribu kuangalia mahali pengine lakini Ngasa alisisitiza kuwa ameambiwa ataendelea kufanya mazoezi hadi ijumaa na anaasilimia kubwa ya kufuzu

Jana usiku niliona katika chombo cha habari kimoja maarufu hapa nchini habari ya Ngasa ilipewa kipaupembele katika habari za michezo na ilieleza ya kwamba Ngasa kashindwa na walizungumza na mtu mmoja yuko huko Uingereza akidai kuwa alienda katika Club ya West Hum na kuambiwa kuwa suala la Ngasa limefungwa yaani ameshindwa.


Baadaye saa 3 usiku nikasikiliza kipindi cha michezo cha redio moja ambao walizungumza na wakala mmoja anayetambuliwa na FIFA hapa nchini ambaye yeye alisema mtu mmoja huwezi kwenda kupata habari za mchezaji kwa Club.
Sasa nani anayesema ukweli?? Ngasa mwenyewe,Vyombo vya habari na ni kipi? Wakala ama watanzania walioko Uingereza?? Mi yangu masikio pia hii ni changamoto kwa vyombo vya habari vya bongo? Ni kiu yangu kubwa kusikia Ngasa anafanikiwa katika hili ili kulete chachu kwa vijana wengine,NAIPENDA NCHI YANGU

1 comment

Anonymous said...

Baada ya Ngassa kushindwa je unaamini vyombo vya habari au uaamini walengwa ambao kwa hii article yako ni watu wa kupenda kuficha mambo ndiyo maana hata waandishi unaosema hauwaelewi wajitahidi kupata ukweli nje ya box. Hii ndiyo Tanzania, kila kitu ni visingizio tu, ukiwa Tanzania please relay on out side of the box facts. Ambazo mimi mara nyingi naziamini, ukiwaambiwa fulani kaiba pesa, wewe fanya uchunguzi wa kina utabaini ukweli lakini ukimuuliza mlengwa kamwe hautapata ukweli.

Mtazamo News . Powered by Blogger.