MTANGAZAJI

MZEE JOSIA PAUL SAGATTI AFARIKI DUNIA


Mnamo tarehe 11 March 2008 majira ya saa saba mchana, Mzee Josia Paul Sagatti(wa kwanza kulia pichani juu) alifariki dunia katika hospitali ya Rufaa Bugando, Jijini Mwanza.

Mzee huyu ni mmoja kati ya waanzilishi wa Kanisa la Kirumba na kwaya ya Kirumba, na amekuwa ni msaada mkubwa sana kwa kwaya mbali mbali za Jijini mwanza, hasa kwaya ya kirumba.

Tunawapa pole wafiwa wote!



1 comment

Anonymous said...

Nimeguswa sana na kifo cha huyu ndugu ambaye nilimfahamu binafsi kwa kuwahi kuimba katika kwaya alokuwa akiiongoza hapo SDA church Kirumba mnamo mwaka1976. Nilimjua kama mtu mwema na mpole sana na pia mchapa kazi hodari aliyependa kujiendeleza daima kielimu. At least tulionana kila baada ya wiki mbili, kando ya shughuli za kanisa, pale TLS (Mwanza Library) nilipokifanya kazi, akija kurudisha au kuazima vitabu, mainly on Accountancy. Natoa rambirambi kwa familia yake yote nikimwomba Bwana awape faraja na amani ambavyo Yeye pekee aweza kutoa. E.Manda, France.

Mtazamo News . Powered by Blogger.