MTANGAZAJI CHIPUKIZI
"Ni kijana mdogo lakini mambo yake ni makubwa" Natumaini familia ya Mzee Fadhili Ngomoi ya mjini Morogoro itakuwa inajivunia kutokana na kubahatika kumpata na kumlea kijana wao mdogo anayesoma darasa la sita katika shule ya msingi ya Agape inayomilikiwa na kanisa la waadventista Morogoro.
Kijana huyu Ngomoi Fadhili(pichani)ameanza kuonesha vipaji alivyonavyo ambavyo ni uimbaji na utangazaji wa vipindi vya redio na hivyo kuna haja kubwa ya kumwendeleza,kwa sasa tayali ameshaanza kusikika akitangaza matangazo ya AWR kwa siku ya jumapili ambayo huwa ni maalum kwa watoto wote wanaosikiliza matangazo hayo.
"Nataka kusoma ili niwe Daktari wa binadamu na baada ya hapo nisomee uchungaji maana ni kazi ninazopenda kuzifanya maishani"anaeleza kijana huyu katika mahojiano nami hivi karibuni hapa studio kabla ya kuanza kumfundisha jinsi ya kutangaza vipindi vya redio.
Kwa wapenzi wa nyimbo za injili subirini kwa hamu kubwa kumsikia katika matangazo yetu akiimba lakini kwa wale waliobahatika kumwona watakubaliana nami kuwa kijana huyu anacho kipaji cha uimbaji ambacho pia kinahitaji kuendelezwa.
Post a Comment