JE WAJUA????????

Anna Ogolla,Rispa Orembe,Lineth Wilfred,Judith Owire,Happy Nyangoe na Milka Owire ni waimbaji wa kike walioanzisha kundi la uimbaji toka jijini Mwanza mwaka 1999 linalojulikana kwa jina la AMAZING GROUP chini ya mwalimu wao wakati huo Godfrey Jonathan ambaye ni mtayarishaji(Producer) wa muziki wa injili wa Morning Star 105.3 FM ya jijini Dar es salaam Tanzania
Kundi hili lilipata waimbaji wengine tofauti na wale wa awali kutokana na baadhi yao kujiunga na masomo na wengine kwenda kutafuta maisha sehemu nyingine.
Kwa sasa waimbaji wanaounda kundi hili lililoanzishwa kwa kusudi la kutoa injili kwa njia ya uimbaji ni Liliani Bomani ambaye ni mwenyekiti,Katibu ni Roda Mkama,Mhazini wa kundi ni Lineth Owire,Matroni Anna Ogolla,Milka Owire ni Mwenyekiti wa Miradi,wengine ni Jane Peter na Happy Nyangoe.
Walimu waliosaidia maendeleo ya kundi hili ni Godfrey Jonathan,Darlington Onditi na Nico Mujaya
Amazing group wanataraji kutoa albamu mbili za nyimbo
Kama unahitaji kuwasiliana na waimbaji hawa tumia anuani yao ya barua pepe: kirumbaadventist@yahoo.co.uk
Post a Comment