MTANGAZAJI

NYUMBANI NI NYUMBANI

Popote pale ninapokuwa sitoweza kusahau BISMARCK ROCK iliyoko katika Ziwa Victoria huko Mwanza,Tanzania hata hivyo mpaka sasa sijapata habari za uhakika kwa nini jiwe hili lilipewa jina hilo pamoja na kusoma historia lakini bado akili yangu haijawa na amani kwa jina hilo naamini siku moja nitampata babu mmoja wa kisukuma nifanya naye mahojiano,kuzungumzia sehemu hii.

Picha hii niliipiga mwaka 2006 nilipoenda nyumbani Mwanza kwa mapumziko kidogo sehemu hii inanikumbusha mbali sana na inanisikitisha kuona kina cha maji kimepungua katika Ziwa hili ambalo linaunganisha nchi za Afrika Mashariki.

Kwa taarifa tu ni kwamba mita chache kutoka katika eneo hili ndipo ilipo shule ya Msingi Nyamagana ambayo nilisoma darasa la "vidudu "kwa sasa shule za awali .

Na pia nilipenda sana kwenda kuvua samaki kwa ndoano wakati wa "ujana wangu siku hizo za miaka ya 47"

Sasa sijui nianzishe kipindi cha TULIKOTOKA hapa AWR naombeni maoni yenu............

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.