NGUVU KAZI YA WAHAMIAJI KWA NCHI ZILIZOENDELEA.
Kadri nchi nyingi zilizoendelea zinavyokabiliwa na ongezeko la idadi ya wazee na kupungua kwa nguvu kazi, ushiriki wa watu katika soko la ajira umekuwa jambo muhimu zaidi, na ni moja ya sababu kuu zinazoongoza sera za uhamiaji.
Katika nchi za Umoja wa Ushirikino wa Maendeleo ya Kiuchumi duniani (OECD), wastani wa ushiriki wa wahamiaji katika nguvu kazi ni asilimia 77, kiwango ambacho ni juu kidogo kuliko asilimia 76 ya watu waliozaliwa katika nchi husika. Katika nchi nyingi, wahamiaji wanashiriki kikamilifu katika soko la ajira kwa kiwango kinacholingana, au hata kuzidi, kile cha wazawa.
Takwimu za Mtazamo wa Uhamiaji wa Kimataifa 2025 zilizotolewa na OECD zinaonyesha viwango vya ushiriki wa nguvu kazi kwa watu waliozaliwa nchi husika na waliozaliwa nje ya nchi katika mataifa ya OECD, yakiwemo Chile, Luxembourg, Marekani, Ujerumani, Canada, Australia, Japan, Uingereza na mengine mengi.
Chile inaonyesha pengo kubwa zaidi linalowanufaisha wahamiaji, likiwa ni tofauti ya Luxembourg pia inajitokeza, ambapo Costa Rica ina mwelekeo unaofanana, huku ushiriki wa wahamiaji unafikia asilimia 74, ikilinganishwa na asilimia 65 ya raia waliozaliwa katika nchi hizo.
Katika baadhi ya nchi zenye uchumi mkubwa barani Ulaya, hali ni tofauti. Nchini Ujerumani, ushiriki wa wazawa ni asilimia 82, ikilinganishwa na asilimia 74 ya wahamiaji. Ingawa Ujerumani inakabiliwa na upungufu wa wafanyakazi na imepanua fursa za uhamiaji wa wataalamu, takribani asilimia 24 ya wahamiaji wa muda mrefu ni wa kibinadamu, ambao mara nyingi hawaingii mara moja katika soko la ajira.
Uholanzi na Uturuki zinaonyesha mapengo makubwa zaidi, ambapo ushiriki wa wazawa katika nguvu kazi unazidi ule wa wahamiaji kwa alama za asilimia 11.2 katika kila nchi.
Kwa ujumla, takwimu hizi zinaonyesha kuwa katika nchi nyingi zilizoendelea, wahamiaji ni sehemu muhimu ya nguvu kazi, na mchango wao unaendelea kuwa nguzo muhimu katika kukabiliana na changamoto za idadi ya watu na uchumi.

.png)
Post a Comment