MTANGAZAJI

KATIBU MKUU WA UN ATAKA MAZUNGUMZO JUMUISHI TANZANIA.

 


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), António Guterres ameitaka Tanzania kuanzisha “mazungumzo ya kitaifa yenye maana na jumuishi” ili kushughulikia sababu za msingi za  vurugu baada ya uchaguzi wa Oktoba 29,2025 na kusababisha  vifo nchini humo.

Kauli hiyo ilitolewa katika mkutano uliofanyika Disemba 14, 2025, ambapo Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Balozi Mahmoud Kombo, aliwasilisha ujumbe maalumu kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Kulingana na taarifa ya serikali ya Tanzania, Bw. Guterres alitambua kwamba sifa ya muda mrefu ya taifa hilo kama “alama ya amani ilijaribiwa” wakati wa uchaguzi wa hivi karibuni. Alisisitiza maslahi ya Umoja wa Mataifa ni kuona Tanzania ikibaki na umoja na kuonyesha msaada kwa UN kwa Tume ya Uchunguzi ya Serikali kuhusu matukio hayo.

Mkutano huu unafanyika huku kukiwa na shinikizo la kimataifa kwa serikali ya Rais Samia. Marekani imeanzisha “mapitio ya kina” ya uhusiano wake wa kidiplomasia na nchi hiyo ya Afrika Mashariki, ikidai mateso ya raia na ukandamizaji wa uhuru wa msingi. Bunge la Ulaya pia limekosoa mauaji baada ya uchaguzi na ukiukwaji wa haki za binadamu.

 Baada ya Uchaguzi wa Oktoba 29 mwaka huu kumeshuhudiwa picha na video mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii kutoka Tanzania zikionesha maandamano, watu kupigwa risasi,na kuchomwa moto kwa  miundo mbinu katika maeneo ya Dar es salaam, Mwanza, Arusha na Songwe  ikiwemo vituo vya bus, magari, vituo vya mafuta na watu wengine kupoteza maisha kwa kile kinachoelezwa kupigwa risasi na polisi nchini humo, huku serikali ya Tanzania ikiwa haijatoa idadi kamili ya waliopoteza maisha

Katika hotuba yake ya Disemba 2, 2025, Rais Samia alieleza hatua zilizochukuwa na vyombo vya usalama kudhibiti vurugu hizo, akihoji “nguvu chache zingekuwa vipi” na kukataa ukosoaji wa nje. 

Wito wa Bw. Guterres wa mazungumzo unasisitiza mtazamo wa jumuiya ya kimataifa katika kutafuta suluhisho la amani na kuhakikisha uwajibikaji kwa vurugu zilizotokea kipindi cha uchaguzi.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.