SHULE YAKOSOLEWA KUZUIA NGUO ZA RANGI NYEUSI
Shule ya Sekondari ya El Paso, Texas, inakabiliwa na ukosoaji baada ya maafisa kutangaza sera mpya ya kanuni ya mavazi ambayo inazuia wanafunzi kuvaa nguo nyeusi "kutoka kichwani hadi miguuni," akiashiria wasiwasi juu ya afya ya akili.
Uamuzi huo ulitangazwa na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Charles,Nick De Santis kabla ya mwaka wa shule ambao ulianza Jumatatu.Barua ilitaja shule hiyo inakataza mavazi meusi kwa sababu ya uhusiano wake "na huzuni na maswala ya afya ya akili au uhalifu.
Jumuiya ya eneo hilo imekosoa kanuni mpya ya mavazi kupitia mtandaoni, ikihoji jinsi rangi ya nguo inavyoathiri ustawi wa kihisia wa watoto.
"Kufanya wanafunzi kuvaa rangi tofauti hakutawafanya kuwa watu tofauti kabisa," , Alexis Contreras, aliiandika.
Baadhi ya wazazi ikiwemo Fabiola Flores, ambaye tayari alifanya manunuzi ya nguo za shule,anasema wanatamani waulizwe kuhusu mabadiliko hayo kabla ya kutekelezwa Tayari tulinunua suruali nyeusi, kwa hiyo tunapaswa kununua tena, suruali za rangi tofauti, Wanapaswa kuuliza,
Norma De La Rosa, Rais wa Chama cha Walimu wa El Paso, alifafanua kwa waandishi wa habari Jumatano kwamba shule hiyo haikupiga marufuku matumizi ya rangi nyeusi.
Post a Comment