MTANGAZAJI

POLISI NA VIONGOZI WA DINI WAIMARISHA ULINZI WA MISIKITI UINGEREZA

 


Baada ya usiku wa siku sita za ghasia za kupinga Uislamu na wahamiaji, na uporaji, mashambulizi dhidi ya polisi na hoteli kuchomwa moto,imamu na viongozi wa jumuiya ya Kiislamu wanashirikiana na polisi kuongeza usalama katika misikiti kote nchini  Uingereza.


Makundi ya siasa kali za mrengo wa kulia yalianzisha maandamano hayo ya ghasia baada ya madai ya uwongo kwamba Mwislamu mzaliwa wa kigeni alihusika na shambulio la kisu la Julai 29 lililoua wasichana watatu na kuwajeruhi watoto wengine wanane na watu wazima wawili katika mji wa kaskazini mwa Uingereza.


Mamlaka nchini humo imemtambua mshukiwa huyo kuwa ni Axel Muganwa Rudakubana mwenye umri wa miaka 17, ambaye alizaliwa Cardiff, anayeripotiwa kuwa na wazazi Wakristo wa Rwanda.


Ghasia hizo zimefichua mgawanyiko kote Uingereza  kuhusu uhamiaji na kuzua wasiwasi kuhusu uwezo wa makundi ya mrengo wenye msimamo mkali wa kulia kwenye mitandao ya kijamii kuzua machafuko kupitia taarifa potofu.


Katika chapisho ambalo sasa limefutwa kwenye X, muuaji alitambuliwa kwa uwongo kama mtafuta hifadhi anayeitwa "Ali al-Shakati" anayejulikana kwa huduma za usalama na mashirika ya afya ya akili. Madai haya ya uwongo yalikuzwa na akaunti zingine za X zilizodai kuwa "vituo vya habari,ambapo moja ya akaunti zinazoelewa kuchochea jambo hilo ikitumia hushtag ya , "End Wokeness," ikiwa ina wafuasi milioni 2.8.


Mwishoni mwa juma lililopita, Ofisi ya Mambo ya Ndani, idara ya baraza la mawaziri inayohusika na usalama wa ndani, ilitangaza kwamba misikiti itapewa ulinzi wa dharura ikiwa iko hatarini, kwa njia ya kikosi cha usalama cha haraka ambacho kitasaidia polisi wa eneo hilo.


Mamia zaidi wameshiriki katika maandamano hayo yenye vurugu, na polisi bado wanapitia picha za CCTV ili kubaini washukiwa. Baadhi ya waandamanaji wa kwanza kushtakiwa walifikishwa mahakamani Jumatatu ya juma hili.

 

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.