MTANGAZAJI

MWANAFUNZI WA SEMINARI AUAWA KWA KUCHOMWA MOTO

 


Washambuliaji wanaoaminika kuwa magaidi kutoka Kabila la Fulani katika eneo la Nigeria wamemuunguza  mwanafunzi wa seminari ya Kikatoliki hadi kufariki hivi karibuni katika jaribio lisilofanikiwa la utekaji nyara, duru zilisema.

Katika shambulio la takriban saa mbili usiku kwenye ofisi ya Kanisa Katoliki la  Raphael huko Fadan Kamantan, Kusini mwa jimbo la Kaduna, chini ya Dayosisi ya Kafanchan, magaidi hawakuweza kuingia katika nyumba ya Paroko waliyetaka kumteka nyara badala yake waliichoma moto, kwa mujibu wa chombo cha habari ACI Africa. 

Kasisi Emmanuel Okolo, na msaidizi wake walifanikiwa kutoroka, lakini moto huo ukaua mwanafunzi wa seminari Na'aman Danlami( 25).

Kasisi wa eneo ambaye alikuwa amefundisha Danlami katika Taasisi ya St. Albert, Kasisi Williams Kaura Abba, aliomba maombi katika ujumbe mfupi wa maandishi kwa Morning Star News.

Abba ameeleza kuwa "Majambazi walienda kufanya utekaji nyara,". "Mapadri  wawili katika nyumba iliyochomwa waliweza kutoroka.

Mkazi wa eneo hilo Andrew Timothy aliambia Morning Star News kwamba mabaki ya Danlami yalipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.

Kundi la Wabunge wa Vyama Vyote nchini Uingereza linalojihusisha na  Uhuru wa Kimataifa au Imani (APPG) lilibainisha  katika ripoti yake ya mwaka  2020 kuwa Kabila la Wafulani huko Nigeria na eneo la Sahel,  wengi wao ni Waislamu wanajumuisha mamia ya koo  nyingi tofauti ambazo hazina misimamo mikali, lakini baadhi ya Wafulani wanafuata itikadi kali za Kiislamu.

Nigeria iliongoza duniani kwa Wakristo waliouawa kwa ajili ya imani yao mwaka 2022, ikiwa na matukio 5,014, kwa mujibu wa ripoti ya Open Doors ya 2023 ya Orodha ya nchi zinazotazamwa Duniani  (WWL)

 

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.