MTANGAZAJI

ALIYETOROKA GEREZANI AKAMATWA

 


Danelo Cavalcante, muuaji aliyepatikana na hatia ambaye alitoroka katika gereza la Pennsylvania nchini Marekani karibu majuma mawili yaliyopita, amekamatwa Septemba 13 mwaka huu, Polisi wamesema, na kuhitimisha msako mkali ambao ulisababisha maeneo ya vijijini ya jimbo hilo, kufunga shule na kuwatia wasiwasi wakaazi wa eneo hilo.

Cavalcante alikamatwa mwendo wa saa 2 asubuhi baada ya ishara joto lake kutambuliwa saa chache mapema na ndege yenye kamera ya picha ya joto,magharibi mwa Pennsylvania , Kaskazini mwa barabara ya Prizer, Luteni Kanali George Bivens wa Polisi wa Jimbo la Pennsylvania amewaambia waandishi wa habari.

Bivens amesema Cavalcante alijaribu kutoroka, akitambaa vichakani  akiwa na bunduki aliyoiba kutoka kwa mwenye nyumba mapema jumahili ambapo  Mbwa wa kupekua aliachiliwa na "kumshinda, akiongeza kwamba Cavalcante aliumwa na mbwa kidogo

Cavalcante, 34, "alikamatwa kwa nguvu" huku akiendelea kufanya purukushani kwa maafisa wa polisi.

 Cavalcante alipelekwa katika kituo cha polisi cha jimbo cha Avondale kuhojiwa. Hatimaye atapelekwa katika gereza ambapo ataanza kutumikia kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia ya mauaji mwezi uliopita.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.