MTANGAZAJI

DKT BARRY BLACK ATIMIZA MIAKA 20 YA UCHAPLENI WA SENETE YA MAREKANI

 


Dkt Barry Clayton  Black ametimiza  miaka 20 akiwa Chapleni wa Seneti ya Marekani huko Washington, D.C. 

Black ambaye atafikisha umri wa miaka 75 mwaka huu, ameshika nafasi hiyo  tangu Juni 27,2003 alifika katika wadhifa huo baada ya kuwa Chapleni Kiongozi wa Jeshi la Wanamaji la Marekani kwa muda wa miaka 27.

Black ndiye mwadventista wa Sabato  wa kwanza kuwa Chapleni Kiongozi wa kwanza wa jeshi la Marekani, na  Mmarekani  Mwafrika wa kwanza  kushika wadhifa huo katika Seneti ya Marekani.

Ikiwa ni sehemu ya majukumu yake, Black hufungua kila kikao cha Seneti kinapofanyika kwa sala, akimwomba Mungu awape wabunge hekima wakati wa kikao hicho cha ngazi ya juu nchini Marekani  ambapo amekuwa mkisisitiza kuwa anawaheshimu watu si kutokana na ajenda za kisiasa.

Katika mahojiano na Mwandishi wa Habari wa The Washington Times Mark A. Kellner anasema Anadhani yeye si mshiriki,"Pamoja na wabunge, sitarajiwi kuweka mawazo yangu katika upande wowote na kutotoa maoni yangu kuhusu masuala mbalimbali na Kwa hiyo, naweza kufanya hivyo na kushiriki nao, na napenda fursa ya kushiriki katika mazungumzo hayo mazuri"

Mnamo mwaka 2017, Black alihutubia wakati huo Rais akiwa ni Donald J. Trump na chumba kilichojaa viongozi wa kisiasa na raia wa Marekani  na viongozi wa kimataifa, akiwemo Mfalme Abdullah II wa Jordan, wakati wa Kiamsha kinywa cha 65 cha Sala ya Kitaifa.

Wakati wa hotuba yake ya wakati wa maombi hayo , ambayo ilitangazwa kitaifa kwenye televisheni,Black alitaja aina ya uhusiano ambao Mungu anataka kuwa nao na wale wanaomkaribia kwa sala, akinukuu maneno ya Yesu kwa wanafunzi Wake katika Yohana 15:16, “Siwaiti tena watumishi Wangu;Nawaita kuwa ni marafiki zangu.

Black ni Mwaadventista wa Sabato wa Pili kushiriki katika maombi hayo ya asubuhi , baada ya aliyekuwa daktari wa upasuaji wa neva na Waziri wa Makazi na Maendeleo ya Miji nchini Marekani  Benjamin S. Carson  kuhutubia kwenye tukio hilo mwaka 2013.

Black ambaye pia mwandishi wa vitabu na Mhubiri  ni mhitimu wa Vyuo Vikuu vya Waadvetista  cha Oakwood  na  Andrews, Chuo Kikuu cha Kati cha North Carolina, Seminari ya Kibaptist ya Mashariki (sasa ikiitwa Seminari ya Thiolojia ya  Palmer),Chuo Kikuu cha Salve Regina, na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Marekani (sasa kikiitwa  Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Alliant).
Chapleni huyo pamoja na kupata shahada tatu za Uzamili za Sanaa katika Uungu, Ushauri nasaha na Uongozi, ana shahada mbili za udaktari,Udaktari wa Uchungaji  na Udaktari wa Falsafa  katika Saikolojia.






No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.